Nchini Uingereza tunaishuhudia klabu ya Manchester City ikiziburuza timu nyingine zinazoshiriki ligi kuu nchini humo na kutabiriwa kuwa huenda ikaweka Historia ya kutwaa ubingwa mapema sana.
Msimu uliopita ulikuwa wa kwanza kwa kocha Pep Guardiola, Manchester City ilimaliza kwenye nafasi ya tatu lakini kocha huyo kutoka Catalunya alisema timu yake ilikuwa na uhaba wa wachezaji na akaahidi kulifanyia kazi tatizo hilo.
Tajiri kutoka Arabuni Sheikh Mansour ndiye anayeimiliki Manchester City na hakumwangusha Guardiola, alimpa pesa zote alizohitaji kukitengeneza kikosi hiki kinachoangamiza karibu kila timu kinachokutana nayo barani Ulaya.
Manchester City sasa inacheza mpira wa aina tofauti kabisa kutokana na umahiri wa kocha wao na wachezaji bora alionao.
Mafanikio haya ya Manchester City yamekuja baada ya uongozi kumuamini Guardiola na kumuachia mamlaka ya kufanya maamuzi juu ya wachezaji anaowataka, maslahi yao na masuala mengine muhimu.
Hivyo ndivyo jinsi timu bora inavyojengwa.
Naiona klabu yangu ya Yanga ikifanya jambo hilo sasa mbali na changamoto za kiuchumu, naamini ni swala la muda tu Yanga itakuwa na mafanikio makubwa barani Afrika.
Aidha utakapokamilika mchakato wa mabadiliko na Yanga kuhamia kwenye mfumo wa hisa, klabu itakuwa na uwezo mkubwa wa kifedha na hapo ndipo tunapotaka twende.
Kwa mara ya kwanza usajili wa Yanga msimu huu kuanzia dirisha kubwa na hata hili dogo lililofungwa jana, wachezaji wote waliosajiliwa walipendekezwa na kocha George Lwandamina.
Yanga imeachana na ile tabia ya zamani ya kila tajiri kusajili mchezaji wake na baadae kulazimisha apangwe hata kama kiwango chake hakiridhishi.
Kama kocha, Lwandamina tayari amedhihirisha ubora wake kwani licha ya kikosi chake kukabiliwa na majeruhi ya muda mrefu kwa wachezaji wake muhimu, ameweza kutengeneza timu ya ushindani kwa kuwatumia wachezaji ambao hawakuwa wakiaminiwa sana.
Ukiangalia kwa ukaribu mambo hayaendi hivyo kwa watani zetu Simba. Msimu huu wamepata hasara kubwa sana kutokana na kufanya usajili usiokuwa na mpangilio.
Wakati wa dirisha dogo la usajili Simba imeachana na wachezaji ambao baadhi yao wamesajiliwa kwa mapesa mengi miezi mitano iliyopita!
Licha ya kutamba kufanya usajili wa mabilioni, Simba ya msimu huu haina tofauti na timu nyingine zinazoshiriki ligi kuu ya Vodacom.
Kwa ujumla, mafanikio ya timu yanahitaji kocha bora, uongozi bora na wachezaji bora.
Sasa ili upate wachezaji bora unahitaji kuwa na fedha.
Lakini kuwa na fedha pekee yake bila ya kuwa na kocha mzuri au uongozi bora hakuwezi kukuletea mafanikio kamwe.

ADVERTISE HERE