Kocha mkuu wa Simba SC, Steve Barker, amesema kikosi chake hakitacheza kwa kujilinda kitakapokutana na Orlando Pirates ya Afrika Kusini apo kesho, bali kitaingia uwanjani kwa dhamira ya kushambulia kuanzia dakika ya kwanza ili kuwania ushindi katika mchezo wa ufunguzi wa Kundi C la Ligi ya Mabingwa Afrika.
Barker ametoa kauli hiyo katika mkutano na waandishi wa habari kuelekea mchezo huo, akieleza kuwa uchambuzi wa wapinzani wake umemsaidia kubaini maeneo yenye nguvu na udhaifu ndani ya kikosi cha Pirates.
Amesema timu hiyo ina uwezo mkubwa wa kufanya mashambulizi ya kushtukiza, lakini pia ina maeneo ambayo Simba inaweza kuyatumia kupata nafasi za kushambulia.
Simba na Pirates zitakutana kesho majira ya saa 10 jioni kwa saa za Afrika mashariki katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam