Young Africans (Yanga SC) leo inatarajia kushuka dimbani kuvaana na MC Alger ya Algeria katika mchezo wa hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika, utakaopigwa Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar, kuanzia saa 10:00 jioni.
Timu hizo zimekutana mara nne katika historia, ambapo Yanga imeshinda mchezo mmoja, MC Alger imeshinda mara mbili, huku mchezo mmoja ukiisha kwa sare.
Matokeo ya mechi zilizopita:
Young Africans 1-0 MC Alger
MC Alger 4-0 Young Africans
MC Alger 2-0 Young Africans
Young Africans 0-0 MC Alger
Kwa rekodi hiyo, MC Alger inaongoza kwa ushindi wa michezo miwili dhidi ya mmoja wa Yanga, huku mchezo mmoja ukiisha kwa sare.
Leo timu hizo zinakutana tena, huku Yanga ikiwa na nafasi ya kuboresha rekodi yake dhidi ya wapinzani hao mbele ya mashabiki wake Zanzibar.