Mshambuliaji wa Al Ahly Tripoli ya Libya, Fiston Mayele, ameonyesha imani kuwa klabu yake ya zamani ya Young Africans (Yanga) ina uwezo wa kufika fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika msimu huu, akitoa mtazamo wake kuhusu safari ya Wananchi katika mashindano hayo.
Mayele ametoa kauli hiyo baada ya mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika kati ya Al Ahly Tripoli na Azam FC, uliomalizika kwa ushindi wa mabao 2-1 kwa timu yake.
Kauli hiyo imekuja wakati Yanga ikiwa kwenye harakati za kuwania mafanikio katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika, ambapo siku ya kesho itakuwa mwenyeji wa MC Alger katika uwanja wa Amaan.