Yanga yapewa mwamuzi Ambongile Tom mchezo dhidi ya MC Alger

Joel JJ By Joel JJ
•
2h ago
Yanga yapewa mwamuzi Ambongile Tom mchezo dhidi ya MC Alger

Shirikisho la Soka Afrika (CAF) limempa jukumu mwamuzi wa kimataifa kutoka Afrika Kusini, Tom Abongile, kusimamia mchezo kati ya Yanga na MC Alger ya Algeria katika hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika (CAFCL).

Abongile ndiye atakayekuwa mwamuzi wa kati katika mtanange huo wa kukata na shoka utakaopigwa Jumamosi, Novemba 28, 2026, kwenye Uwanja wa New Amaan Complex, visiwani Zanzibar.

Huo utakuwa mchezo wa kwanza kwa timu hizo katika Kundi B, huku kila upande ukiwa na dhamira ya kuanza kampeni yake kwa kuvuna pointi tatu muhimu katika harakati za kusaka tiketi ya robo fainali.

Mwamuzi huyo kutoka Afrika Kusini atakuwa na jukumu la kuhakikisha sheria 17 za mchezo wa soka zinazingatiwa katika pambano hilo linalotarajiwa kuwa na ushindani mkali kutokana na historia ya timu hizo.

YANGA INATAKA KULIPA KISASI

Mbali na umuhimu wa pointi tatu, mchezo huo unabeba kumbukumbu chungu kwa Wananchi baada ya MC Alger kuzima ndoto zao za kutinga robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika misimu miwili iliyopita.

Katika msimu huo, Yanga ilikubali kipigo cha mabao 2-0 nchini Algeria kabla ya kulazimishwa sare tasa ya 0-0 katika mchezo wa marudiano uliopigwa kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.

Wananchi walihitaji ushindi pekee ili kusonga mbele, lakini walishindwa kuutumia vyema uwanja wa nyumbani.

Safari hii, kikosi cha Kocha Mkuu Fadlu Davids kina nafasi nyingine ya kuandika historia mpya dhidi ya wapinzani hao kutoka Kaskazini mwa Afrika.

Wakati Fadlu akiweka wazi mikakati yake ya kushinda michezo yote ya nyumbani katika hatua ya makundi, MC Alger ndiyo itakuwa mtihani wake wa kwanza katika kutimiza malengo hayo.

More Stories

Huyu hapa pilato wa mechi kati ya simba dhidi ya Orlando Pirates
Huyu hapa pilato wa mechi kati ya simba dhidi ya Orlando Pirates
30m ago
READ MORE →
Kisa Musiala, Kimmich aukosoa uongozi wa Bayern munich
Kisa Musiala, Kimmich aukosoa uongozi wa Bayern munich
1h ago
READ MORE →
Orlando Pirates yawasili Dar es Salaam kuikabili Simba SC
Orlando Pirates yawasili Dar es Salaam kuikabili Simba SC
2h ago
READ MORE →
Al Ahly yaanza upya: Benchi jipya la ufundi laidhinishwa, baadhi ya wachezaji kuuzwa
Al Ahly yaanza upya: Benchi jipya la ufundi laidhinishwa, baadhi ya wachezaji kuuzwa
2h ago
READ MORE →
Azam Fc vs Al Ahly Tripoli, hapatoshi Zanzibar
Azam Fc vs Al Ahly Tripoli, hapatoshi Zanzibar
2h ago
READ MORE →
Pirates yawasili Dar mapema tayari kuikabili Simba
Pirates yawasili Dar mapema tayari kuikabili Simba
2h ago
READ MORE →
UCL: Liverpool yang’ara, Bayern yapigwa huku PSG na Man United wakiambulia sare
UCL: Liverpool yang’ara, Bayern yapigwa huku PSG na Man United wakiambulia sare
12h ago
READ MORE →
Ofisi za CAF zazinduliwa rasmi Dar es salaam
Ofisi za CAF zazinduliwa rasmi Dar es salaam
19h ago
READ MORE →
BREAKING: Raheem Sterling ahukumiwa kifungo cha miezi 12 jela kwa makosa ya barabarani
BREAKING: Raheem Sterling ahukumiwa kifungo cha miezi 12 jela kwa makosa ya barabarani
21h ago
READ MORE →
Tetesi za usajili Ulaya: Liverpool, Arsenal na Man United kuwania nyota mbalimbali Januari
Tetesi za usajili Ulaya: Liverpool, Arsenal na Man United kuwania nyota mbalimbali Januari
1d ago
READ MORE →