Mshambuliaji wa zamani wa Chelsea, Liverpool, na Man City, Raheem Sterling, amehukumiwa kifungo cha miezi 12 jela baada ya kukiri makosa yanayohusiana na uendeshaji hatari wa gari na kumiliki gesi ya Nitrous Oxide.
Hata hivyo, adhabu hiyo imesimamishwa kwa kipindi cha miezi 18, ikimaanisha hatalazimika kwenda gerezani kwa sasa endapo atazingatia masharti ya adhabu hiyo.
Kwa mujibu wa BBC, Sterling alikiri kuendesha gari kwa hatari katika barabara za M3, M25, A327 na Minley Road. Pia alikiri kumiliki Nitrous Oxide, dawa iliyowekwa katika kundi la Class C, kwa madhumuni ya kuivuta kinyume cha sheria, pamoja na kushindwa kutoa sampuli kwa ajili ya uchunguzi.