Burudani ya soka la vilabu barani Ulaya inarejea leo kwa michezo mikali inayotarajiwa kuwapa mashabiki burudani ya aina yake. Ligi Kuu England na LaLiga zinaendelea huku timu zikisaka pointi muhimu katika mbio za ubingwa na nafasi za juu kwenye msimamo.
Ligi Kuu England
Manchester City itakuwa mwenyeji wa Fulham katika dimba la Etihad Stadium kuanzia saa 15:30 kwa saa za Afrika Mashariki, ikiwa ni mchezo wa mapema wa siku hiyo.
Bournemouth itakutana na Nottingham Forest katika dimba la Vitality Stadium saa 18:00, huku Aston Villa ikiikaribisha Sunderland katika dimba la Villa Park muda huohuo.
Chelsea itakuwa na kibarua dhidi ya Leeds United katika dimba la Stamford Bridge saa 18:00, wakati Tottenham Hotspur ikitarajiwa kukutana na Ipswich Town katika dimba la Tottenham Hotspur Stadium muda huohuo.
Mchezo unaosubiriwa kwa hamu zaidi ni kati ya Newcastle United na Arsenal, utakaopigwa katika dimba la St James’ Park saa 20:30. Arsenal itakuwa na dhamira ya kuondoka na pointi muhimu katika uwanja mgumu wa Newcastle.
LaLiga
Real Madrid itakuwa mwenyeji wa Celta Vigo katika dimba la Santiago Bernabeu, katika mchezo muhimu kwa mbio za kuwania ubingwa wa LaLiga. Los Blancos wanahitaji ushindi ili kuendelea kuisogelea Barcelona, ambayo kesho itakuwa na mtihani dhidi ya Villarreal.
Super Weekend imewadia. Ni muda wa burudani, ushindani na vita ya pointi muhimu.