Kocha Msaidizi wa Young Africans SC, Simo Dladla, ameachana na klabu hiyo kwa makubaliano ya pande zote mbili.
Dladla raia wa Afrika Kusini ameondoka Yanga baada ya kupokea ofa ya kwenda kuwa kocha wa klabu ya Richards Bay FC inayoshiriki soka nchini humo.
Hatua hiyo inamrejesha Dladla katika soka la nyumbani kwake Afrika Kusini, baada ya kipindi alichokuwa akihudumu katika benchi la ufundi la Yanga.