Hersi afafanua sababu za kuchelewa kwa ujenzi wa uwanja wa Yanga, ataja hatua zilizofikiwa

Xtra 90 Media By Xtra 90 Media
β€’
2d ago
Hersi afafanua sababu za kuchelewa kwa ujenzi wa uwanja wa Yanga, ataja hatua zilizofikiwa

Rais wa Young Africans SC, Eng. Hersi Said, amefafanua sababu zilizochelewesha kuanza kwa ujenzi wa uwanja wa klabu hiyo, akisema walilazimika kukamilisha taratibu za kisheria na kiutawala kabla ya kuanza utekelezaji wa mradi huo kwa kushirikiana na GSM Group.

Hersi amesema licha ya klabu kutangaza ushirikiano na GSM Group na kufikia makubaliano ya uwekezaji, ujenzi haukuweza kuanza mara moja kwa sababu kulikuwa na taratibu muhimu zilizopaswa kufuatwa kuhusu umiliki wa ardhi, ridhaa ya wanachama na vibali vinavyohitajika. Ameeleza kuwa klabu ilifanya vikao kadhaa na ofisi ya Kabidhi Wasii Mkuu wa Serikali na kutoa nyaraka pamoja na ufafanuzi uliohitajika.

Amesema katika kutafuta mfumo bora wa kisheria na kiutendaji utakaolinda maslahi ya klabu na mwekezaji, walipata nafasi ya kukutana na Mwanasheria Mkuu wa Serikali pamoja na timu yake ya wataalamu. Katika kikao hicho, waliwasilishwa tathmini na njia tatu zinazoweza kutumika kutekeleza mradi huo.

Kwa mujibu wa Hersi, mojawapo ya njia hizo ni mfumo wa ushirikiano wa kibiashara kupitia kampuni maalumu ya mradi (SPV), pamoja na makubaliano ya uwekezaji yanayojulikana kama Shareholders Agreement (SHA). Amesema njia hiyo ilikuwa tayari imefanyiwa tathmini na Kamati ya Utendaji pamoja na Baraza la Wadhamini, lakini walihitaji pia kuchambua mapendekezo mengine mawili yaliyotolewa na Serikali.

Hersi amefichua kuwa Novemba 17, 2026, klabu ilipokea barua kutoka kwa Kabidhi Wasii Mkuu wa Serikali yenye mwongozo rasmi kuhusu namna ya kuendelea na utekelezaji wa mradi huo. Baada ya kupitia njia zote tatu na kufanya mashauriano na Baraza la Wadhamini, Kamati ya Utendaji ilikubaliana kuendelea na pendekezo la kuhamisha ardhi ya mradi kutoka kwenye mfumo wa umiliki wa wadhamini kwenda katika kampuni ya Jangwani Complex Limited.

Amesema mwongozo wa Serikali umeweka mkazo katika maeneo muhimu ya kulinda maslahi ya Young Africans na GSM Group. Eneo la kwanza ni kuhakikisha ardhi ya klabu haitatumika kama dhamana ya kupata mikopo au madeni ya mwekezaji. Hersi amesisitiza kuwa GSM Group imeonyesha uwezo wa kifedha na kutenga rasilimali kwa ajili ya ujenzi wa uwanja bila kutegemea mkopo utakaotokana na kutumia ardhi ya Yanga kama dhamana.

Eneo la pili linahusu kutenganisha madeni na changamoto za kibiashara za kila upande na mali za mradi wa Jangwani Complex Limited. Hersi amesema changamoto za kifedha zinazoweza kuikumba Yanga katika shughuli zake nyingine hazipaswi kuathiri mali za mradi huo, vivyo hivyo kwa GSM Group. Lengo ni kuhakikisha kampuni ya mradi inabaki salama na inaendeshwa kwa mfumo wake wa kisheria na kifedha.

Hersi amesisitiza kuwa hatua hizo zinalenga kulinda mali ya klabu na kuhakikisha uwekezaji unatekelezwa kwa usalama wa muda mrefu. Ameishukuru Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Kabidhi Wasii Mkuu wa Serikali kwa mwongozo na ushirikiano walioutoa, akieleza kuwa mradi huo una umuhimu mkubwa katika historia ya Yanga na maendeleo ya miundombinu ya soka nchini.

More Stories

Singida Black Stars yaichapa Azam 4-2, Sowah atupia mabao mawili
Singida Black Stars yaichapa Azam 4-2, Sowah atupia mabao mawili
6h ago
READ MORE β†’
Shalulile, Toure waizamisha Polisi Tanzania, Yanga yashinda 2-0 Moshi
Shalulile, Toure waizamisha Polisi Tanzania, Yanga yashinda 2-0 Moshi
10h ago
READ MORE β†’
Highlights : Polisi Tanzania 0-2 Yanga, Ligi Kuu
Highlights : Polisi Tanzania 0-2 Yanga, Ligi Kuu
11h ago
READ MORE β†’
Spain kukutana na Ufaransa, England kukabiliana na Norway robo fainali Nations League
Spain kukutana na Ufaransa, England kukabiliana na Norway robo fainali Nations League
12h ago
READ MORE β†’
Ahmad Ally aitangazia vita Simba
Ahmad Ally aitangazia vita Simba
14h ago
READ MORE β†’
Barker afunguka maandalizi ya kuikabili JKT Tanzania
Barker afunguka maandalizi ya kuikabili JKT Tanzania
14h ago
READ MORE β†’
Mourinho aeleza msimamo wake kuhusu Vinicius Real Madrid
Mourinho aeleza msimamo wake kuhusu Vinicius Real Madrid
15h ago
READ MORE β†’
Walionufaika na waliopoteza wakati wa mapumziko ya mechi za kimataifa.
Walionufaika na waliopoteza wakati wa mapumziko ya mechi za kimataifa.
16h ago
READ MORE β†’
Real Madrid kuongeza mikataba ya Courtois na Valverde
Real Madrid kuongeza mikataba ya Courtois na Valverde
17h ago
READ MORE β†’
Ligi kuu ya NBC kuendelea leo: Yanga Moshi, Azam na Singida Bs kukutana Chamazi
Ligi kuu ya NBC kuendelea leo: Yanga Moshi, Azam na Singida Bs kukutana Chamazi
20h ago
READ MORE β†’