Beki wa Simba SC na Timu ya Taifa ya Tanzania, Nathaniel Chilambo, anatarajiwa kuwa nje ya uwanja kwa kipindi cha wiki tatu hadi nne baada ya kupata jeraha la mishipa wakati wa mchezo wa kufuzu AFCON 2027 dhidi ya Nigeria.
Kwa mujibu wa taarifa baada ya uchunguzi wa kitabibu umebaini ukubwa wa jeraha hilo na kuthibitisha kuwa beki huyo atahitaji muda huo kurejea katika hali nzuri ya kucheza. Hata hivyo, Simba SC haijatoa taarifa rasmi kuhusu hali ya kiafya ya mchezaji huyo.
Chilambo alipata jeraha hilo katika mchezo wa marudiano dhidi ya Nigeria apo jana, ambapo alionekana akipatiwa huduma ya kwanza na wahudumu wa afya pembeni mwa uwanja kabla ya kushindwa kuendelea na mchezo.
Jeraha hilo linakuwa pigo kwa Simba, hasa ikizingatiwa kuwa kipindi cha kupona kwake kinaingiliana na maandalizi ya kuanza kwa hatua ya makundi ya mashindano ya klabu Afrika, inayotarajiwa kuanza Novemba 27, 2026. Hali hiyo pia inamaanisha Taifa Stars italazimika kukosa huduma ya beki huyo katika kipindi cha kurejea kwa wachezaji kwenye majukumu ya timu zao.