Vinicius Jr arejea kwa kishindo, afunga mabao matano katika mechi mbili za Brazil

Xtra 90 Media By Xtra 90 Media
β€’
3d ago
Vinicius Jr arejea kwa kishindo, afunga mabao matano katika mechi mbili za Brazil

Mshambuliaji wa Brazil na Real Madrid, Vinicius Jr, ameonyesha kurejea kwenye kiwango bora baada ya kufunga mabao matano katika michezo miwili iliyopita ya timu yake ya taifa, akianza kwa mabao mawili dhidi ya Japan kabla ya kupiga hat trick dhidi ya Singapore.

Katika mchezo dhidi ya Singapore, Vinicius aliiba show kwa kufunga mabao matatu ndani ya dakika 21 pekee. Alianza kwa bao dakika ya tisa, akaongeza la pili dakika ya 15 na kukamilisha hat trick dakika ya 21, akionyesha makali yaliyomfanya kuwa mmoja wa washambuliaji hatari barani Ulaya.

Kabla ya hapo, alifunga mabao mawili katika mchezo dhidi ya Japan licha ya Brazil kupoteza kwa mabao 3-2. Bao lake la kwanza lilikuwa shuti kali la nje ya eneo la hatari dakika ya 33, kabla ya kuongeza la pili dakika ya 75 kwa shuti la chini baada ya kuingia kutoka upande wa kushoto.

Mabao hayo matano yamekuja wakati Vinicius akikabiliwa na changamoto ya kiwango katika klabu yake ya Real Madrid, ambako amekuwa akikosolewa kutokana na kupungua kwa mchango wake wa mabao. Katika michezo 12 aliyocheza msimu huu, alikuwa amefunga bao moja na kutoa asisti tatu.

Akizungumza kabla ya mchezo dhidi ya Singapore, Vinicius alikiri kuwa maandalizi yake baada ya Kombe la Dunia 2026 hayakuwa mazuri kama miaka iliyopita. Alieleza kuwa kutolewa mapema kwa Brazil kulimuathiri, hivyo alitumia mapumziko yake kupumzika na kuwa pamoja na familia badala ya kufanya mazoezi kwa kiwango alichozoea.

Pia alikiri kuwa mjadala kuhusu mkataba wake mpya na Real Madrid pamoja na kuvutiwa kwake na vilabu vingine ulimletea changamoto ya kiakili na kuathiri umakini wake mwanzoni mwa msimu.

Hata hivyo, Vinicius amesema anaamini ana uwezo wa kurejea kwenye kiwango chake bora, akitolea mfano msimu uliopita ambapo alianza kwa kusuasua lakini baadaye akafunga zaidi ya mabao 20. Ameeleza kuwa anaendelea kufanya kazi ili kuboresha kiwango chake na kuwa tayari kwa michezo muhimu.

Sasa mabao matano katika mechi mbili za Brazil yanampa Vinicius nafasi ya kurejesha kujiamini kabla ya kurejea Real Madrid. Changamoto kubwa iliyopo mbele yake ni kuendeleza makali hayo akiwa klabuni na kuthibitisha kuwa kipindi kigumu alichopitia kilikuwa cha muda tu.

More Stories

Singida Black Stars yaichapa Azam 4-2, Sowah atupia mabao mawili
Singida Black Stars yaichapa Azam 4-2, Sowah atupia mabao mawili
6h ago
READ MORE β†’
Shalulile, Toure waizamisha Polisi Tanzania, Yanga yashinda 2-0 Moshi
Shalulile, Toure waizamisha Polisi Tanzania, Yanga yashinda 2-0 Moshi
10h ago
READ MORE β†’
Highlights : Polisi Tanzania 0-2 Yanga, Ligi Kuu
Highlights : Polisi Tanzania 0-2 Yanga, Ligi Kuu
11h ago
READ MORE β†’
Spain kukutana na Ufaransa, England kukabiliana na Norway robo fainali Nations League
Spain kukutana na Ufaransa, England kukabiliana na Norway robo fainali Nations League
12h ago
READ MORE β†’
Ahmad Ally aitangazia vita Simba
Ahmad Ally aitangazia vita Simba
14h ago
READ MORE β†’
Barker afunguka maandalizi ya kuikabili JKT Tanzania
Barker afunguka maandalizi ya kuikabili JKT Tanzania
14h ago
READ MORE β†’
Mourinho aeleza msimamo wake kuhusu Vinicius Real Madrid
Mourinho aeleza msimamo wake kuhusu Vinicius Real Madrid
15h ago
READ MORE β†’
Walionufaika na waliopoteza wakati wa mapumziko ya mechi za kimataifa.
Walionufaika na waliopoteza wakati wa mapumziko ya mechi za kimataifa.
16h ago
READ MORE β†’
Real Madrid kuongeza mikataba ya Courtois na Valverde
Real Madrid kuongeza mikataba ya Courtois na Valverde
17h ago
READ MORE β†’
Ligi kuu ya NBC kuendelea leo: Yanga Moshi, Azam na Singida Bs kukutana Chamazi
Ligi kuu ya NBC kuendelea leo: Yanga Moshi, Azam na Singida Bs kukutana Chamazi
20h ago
READ MORE β†’