Mshambuliaji Romelu Lukaku ametangaza kustaafu kuichezea timu ya taifa ya Belgium baada ya kuitumikia kwa kipindi cha miaka 16.
Kupitia ujumbe wake, Lukaku amesema ametoa kila alichokuwa nacho kwa timu ya taifa na kupitia hisia mbalimbali katika safari yake, huku akiwashukuru wachezaji wenzake, makocha na mashabiki kwa sapoti yao.
Lukaku amesema anajivunia kuiwakilisha nchi yake katika fainali nne za Kombe la Dunia na michuano mitatu ya Mataifa ya Ulaya.
Nyota huyo amesema amefikia uamuzi huo akiwa na amani moyoni na hatasahau nyakati alizopata akiwa na timu ya taifa ya Belgium.