England yaivunja rekodi ya Spain ya mechi 43 bila kupoteza, Italia yatupwa nje ya Nations League

Xtra 90 Media By Xtra 90 Media
β€’
5d ago
England yaivunja rekodi ya Spain ya mechi 43 bila kupoteza, Italia yatupwa nje ya Nations League

England imepata ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya mabingwa wa dunia Spain katika mchezo uliopigwa mjini Madrid, huku matokeo hayo yakimaliza rekodi ya Spain ya kutopoteza mechi 43 mfululizo.

Harry Kane aliipa England bao la kwanza kwa penalti dakika ya 45 kabla ya Ezri Konsa kuongeza la pili dakika ya 53. Dakika nne baadaye, Ben White aliandika bao la tatu na kuifanya England kuwa mbele kwa mabao 3-0.

Spain haikukata tamaa, ikaanza kurejea kupitia Mikel Oyarzabal aliyefunga kwa penalti dakika ya 65, kabla ya Nico Williams kuongeza bao la pili dakika ya 75. Hata hivyo, England ilifanikiwa kulinda ushindi huo licha ya kumaliza mchezo ikiwa na wachezaji 10.

Katika mchezo mwingine, Italia imeondolewa rasmi kwenye Nations League baada ya kukubali kichapo cha mabao 4-1 kutoka kwa Ubelgiji. Italia ilianza kwa kupata bao kupitia Esposito dakika ya 11, lakini Ubelgiji ilijibu kwa mabao ya Decuyper dakika ya 15, Ngoy dakika ya 22 na Doku dakika ya 26. Moreira alifunga bao la nne dakika ya 80 na kukamilisha ushindi huo.

Ufaransa nayo iliibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Uturuki. Bao la kujifunga la Topçu dakika ya 49 na bao la Kroupi dakika ya 80 yaliipa Ufaransa ushindi, huku Bardakci akiifungia Uturuki dakika ya 90.

Kwa upande mwingine, Croatia iliifunga Czechia mabao 2-1. Perisic aliipa Croatia bao la mapema dakika ya pili, kabla ya Hlozek kusawazisha dakika ya 85. Majer aliihakikishia Croatia ushindi kwa bao la dakika ya 87.

More Stories

Singida Black Stars yaichapa Azam 4-2, Sowah atupia mabao mawili
Singida Black Stars yaichapa Azam 4-2, Sowah atupia mabao mawili
6h ago
READ MORE β†’
Shalulile, Toure waizamisha Polisi Tanzania, Yanga yashinda 2-0 Moshi
Shalulile, Toure waizamisha Polisi Tanzania, Yanga yashinda 2-0 Moshi
10h ago
READ MORE β†’
Highlights : Polisi Tanzania 0-2 Yanga, Ligi Kuu
Highlights : Polisi Tanzania 0-2 Yanga, Ligi Kuu
11h ago
READ MORE β†’
Spain kukutana na Ufaransa, England kukabiliana na Norway robo fainali Nations League
Spain kukutana na Ufaransa, England kukabiliana na Norway robo fainali Nations League
12h ago
READ MORE β†’
Ahmad Ally aitangazia vita Simba
Ahmad Ally aitangazia vita Simba
14h ago
READ MORE β†’
Barker afunguka maandalizi ya kuikabili JKT Tanzania
Barker afunguka maandalizi ya kuikabili JKT Tanzania
14h ago
READ MORE β†’
Mourinho aeleza msimamo wake kuhusu Vinicius Real Madrid
Mourinho aeleza msimamo wake kuhusu Vinicius Real Madrid
15h ago
READ MORE β†’
Walionufaika na waliopoteza wakati wa mapumziko ya mechi za kimataifa.
Walionufaika na waliopoteza wakati wa mapumziko ya mechi za kimataifa.
16h ago
READ MORE β†’
Real Madrid kuongeza mikataba ya Courtois na Valverde
Real Madrid kuongeza mikataba ya Courtois na Valverde
17h ago
READ MORE β†’
Ligi kuu ya NBC kuendelea leo: Yanga Moshi, Azam na Singida Bs kukutana Chamazi
Ligi kuu ya NBC kuendelea leo: Yanga Moshi, Azam na Singida Bs kukutana Chamazi
20h ago
READ MORE β†’