Kocha wa Timu ya Taifa ya Ureno, Jorge Jesus, ameonyesha kutoridhishwa na maswali yanayoendelea kumhusu Cristiano Ronaldo, hali iliyojitokeza baada ya timu yake kupokea kipigo cha mabao 4-1 kutoka Denmark katika mchezo uliochezwa bila uwepo wa nyota huyo mkongwe.
Akizungumza na waandishi wa habari baada ya mchezo huo, Jesus alionekana kukerwa na namna maswali kuhusu Ronaldo yalivyoendelea kutawala mazungumzo licha ya mwelekeo wa mchezo na matokeo yaliyopatikana.
“Namkumbuka kwa lipi? Siyo kama bado yupo hapa! Hayupo tena kwenye timu ya taifa, nini kinakosekana? Kitu pekee ambacho kinaweza kuwa kinakosekana ni uwepo wa Cristiano hapa kwa ajili ya kunipa kampuni tu,” alisema Jesus.
Kwa upande mwingine, kipigo cha mabao 4-1 dhidi ya Denmark kimeongeza presha kwa Jesus na kikosi chake, huku maswali kuhusu Ronaldo yakiendelea kuwa sehemu ya mjadala unaozunguka timu hiyo.