Nicolas Jackson atwaa tuzo ya mchezaji bora wa mwezi Oktoba EPL

Xtra 90 Media By Xtra 90 Media
β€’
13 Nov 2026
Nicolas Jackson atwaa tuzo ya mchezaji bora wa mwezi Oktoba EPL

Mshambuliaji wa Aston Villa, Nicolas Jackson, ametwaa tuzo ya mchezaji bora wa mwezi (EA SPORTS Player of the Month) kwa mwezi Oktoba baada ya kuonyesha kiwango cha kuvutia katika Ligi Kuu England, akifunga mabao manne katika michezo minne aliyocheza ndani ya mwezi huo.

Jackson alianza mwezi kwa kufunga bao la kusawazisha katika sare ya mabao 2-2 dhidi ya Brentford, kabla ya kuonyesha kiwango kizuri katika ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Newcastle United ugenini. Aliendelea kung’ara kwa kufunga mabao mawili katika ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Manchester City, kabla ya kufunga bao la kwanza katika sare ya 1-1 dhidi ya Fulham na kukamilisha mwezi akiwa na mabao manne.

Ushindi wa Aston Villa dhidi ya Manchester City ulikuwa miongoni mwa matokeo muhimu katika mwezi huo, kwani Villa ikawa timu ya kwanza kuizuia Manchester City ya kocha Enzo Maresca kupata ushindi katika msimu huo. Jackson alikuwa sehemu muhimu ya mafanikio hayo baada ya kufunga mabao yote mawili yaliyoipa timu yake ushindi.

Kwa kutwaa tuzo hiyo, Jackson anaweka historia akiwa mchezaji wa kwanza wa Aston Villa kushinda tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwezi tangu Christian Benteke aliyefanikiwa kufanya hivyo Aprili 2015. Pia anakuwa mchezaji wa nne kutoka Senegal kutwaa tuzo hiyo, akifuata nyayo za Sadio Mané ambaye aliibuka mshindi Novemba 2019.

Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 25 aliwashinda wagombea wengine waliokuwa kwenye orodha ya mwisho ya wachezaji nane, akiwemo Evanilson wa Bournemouth, Ezri Konsa wa Arsenal, Declan Rice wa Arsenal, Jack Rudoni wa Coventry City, Jan Paul van Hecke wa Tottenham Hotspur, Bart Verbruggen na Luka Vuskovic wa Brighton.

Tuzo hiyo inaongeza mafanikio yake binafsi tangu kurejea kwenye ushindani wa Premier League, huku akijiweka katika nafasi nzuri ya kuwania tuzo na heshima zaidi kutokana na kiwango chake cha ufungaji mabao.

More Stories

Singida Black Stars yaichapa Azam 4-2, Sowah atupia mabao mawili
Singida Black Stars yaichapa Azam 4-2, Sowah atupia mabao mawili
6h ago
READ MORE β†’
Shalulile, Toure waizamisha Polisi Tanzania, Yanga yashinda 2-0 Moshi
Shalulile, Toure waizamisha Polisi Tanzania, Yanga yashinda 2-0 Moshi
10h ago
READ MORE β†’
Highlights : Polisi Tanzania 0-2 Yanga, Ligi Kuu
Highlights : Polisi Tanzania 0-2 Yanga, Ligi Kuu
11h ago
READ MORE β†’
Spain kukutana na Ufaransa, England kukabiliana na Norway robo fainali Nations League
Spain kukutana na Ufaransa, England kukabiliana na Norway robo fainali Nations League
12h ago
READ MORE β†’
Ahmad Ally aitangazia vita Simba
Ahmad Ally aitangazia vita Simba
14h ago
READ MORE β†’
Barker afunguka maandalizi ya kuikabili JKT Tanzania
Barker afunguka maandalizi ya kuikabili JKT Tanzania
14h ago
READ MORE β†’
Mourinho aeleza msimamo wake kuhusu Vinicius Real Madrid
Mourinho aeleza msimamo wake kuhusu Vinicius Real Madrid
15h ago
READ MORE β†’
Walionufaika na waliopoteza wakati wa mapumziko ya mechi za kimataifa.
Walionufaika na waliopoteza wakati wa mapumziko ya mechi za kimataifa.
16h ago
READ MORE β†’
Real Madrid kuongeza mikataba ya Courtois na Valverde
Real Madrid kuongeza mikataba ya Courtois na Valverde
17h ago
READ MORE β†’
Ligi kuu ya NBC kuendelea leo: Yanga Moshi, Azam na Singida Bs kukutana Chamazi
Ligi kuu ya NBC kuendelea leo: Yanga Moshi, Azam na Singida Bs kukutana Chamazi
20h ago
READ MORE β†’