Kiungo mshambuliaji wa timu ya taifa ya Ufaransa na klabu ya Paris Saint-Germain, Désiré Doué, amelazimika kutolewa uwanjani baada ya kupata jeraha la meno kufuatia kugongwa usoni katika mchezo dhidi ya Italia.
Tukio hilo lilitokea wakati kiungo wa Italia, Davide Frattesi, alipomkuta Doué kwa kiwiko usoni walipokuwa wakigombea mpira. Pigo hilo lilisababisha moja ya meno ya mbele ya Doué kutoka katika nafasi yake ya kawaida.
Baada ya tukio hilo, Doué alionekana kupata maumivu na kushindwa kuendelea na mchezo, hali iliyolazimu benchi la ufundi la Ufaransa kumtoa uwanjani na kumuingiza mchezaji mwingine kuchukua nafasi yake.
Jeraha hilo limekuwa miongoni mwa matukio yaliyojitokeza katika mchezo huo wa kimataifa, ambao pia haukuwa na matokeo mazuri kwa Ufaransa baada ya kukubali kipigo cha mabao 3-1 kutoka kwa Italia. Hadi sasa, hali ya jeraha la Doué na muda atakaokaa nje ya uwanja bado unasubiriwa kufahamika.