Kipa wa FC Andorra, Jesús Owono, bado anaendelea kupitia kipindi kigumu kufuatia kifo cha mshambuliaji wa CD Tenerife, Jesús de Miguel, huku taarifa zikieleza kuwa amekuwa akijitenga na shughuli za kawaida na mara chache hutoka nyumbani kwake.
Kwa mujibu wa Marca, Owono anapata msaada wa kisaikolojia na huduma za kitabibu kutoka kwa wataalamu wa klabu yake, lakini bado hajarejea kwenye mazoezi ya timu.
Aidha, kipa huyo ameomba nafasi ya kuzungumza na familia ya marehemu Jesús de Miguel, hata hivyo familia hiyo imeomba muda zaidi kabla ya kukutana naye.
Ikumbukwe, Owono alihusika katika tukio la kugongana na De Miguel katika mchezo wa Ligi Daraja la Pili nchini Hispania kati ya Tenerife na FC Andorra, uliochezwa Novemba 2, 2026. Tukio hilo lilitokea dakika za nyongeza wakati matokeo yakiwa 2-2, ambapo Owono alitoka golini kuwania mpira na kugongana na mshambuliaji huyo. Kipa huyo alionyeshwa kadi nyekundu, huku De Miguel akipata matatizo makubwa ya kiafya na baadaye kufariki dunia akiwa hospitalini.