Mchezo wa kusisimua wa Ligi Kuu England (EPL) kati ya Manchester United na Aston Villa umemalizika kwa sare ya mabao 4-4, katika pambano lililoshuhudia mabadiliko makubwa ya matokeo.
Aston Villa ilianza kwa kasi na kupata mabao mawili ndani ya dakika 5 za mwanzo, dakika ya 1 kupitia winga wao Alysson na 4 Kupitia Jackson, na kuongoza kwa 2-0. Hata hivyo, Manchester United ilirejea mchezoni kwa kufunga mabao mawili dakika ya 16 kupitia penalti ya Bruno Fernandez na dakika ya 44 kupitia kiungo Tielemans na kufanya matokeo kuwa 2-2 kabla ya mapumziko.
Kipindi cha pili kilianza kwa Aston Villa kuongeza kasi na kufunga mabao mawili dakika ya 48 na 53, na kuifanya iongoze kwa 4-2. United haikukata tamaa, ikasaka mabao ya kusawazisha hadi dakika za mwisho.
Katika dakika za nyongeza, Manchester United ilifanikiwa kufunga mabao mawili dakika ya 90+2 Joshua Zirkzee na 90+6 kupitia winga Patrick Dorgu na kuokoa pointi moja katika mchezo huo uliokuwa na msisimko mkubwa.
Matokeo ya mwisho ni Manchester United 4-4 Aston Villa, sare iliyowapa mashabiki burudani ya aina yake na kuonyesha uwezo wa United kurejea hata ikiwa nyuma kwa mabao mawili.