Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) limewateua waamuzi wanne kutoka Tanzania kusimamia mchezo wa kufuzu michuano ya Mataifa ya Afrika (AFCON 2027) kati ya Equatorial Guinea na Zimbabwe.
Waamuzi waliopata nafasi hiyo ni Ahmed Arajiga, Hamdan Ally, Ally Ramadhani na Nasir Salum, ambao watakuwa sehemu ya timu ya waamuzi katika mchezo huo.
Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Novemba 12, 2026, katika Uwanja wa Omnisports Ahmadou Ahidjo jijini Yaoundé, Cameroon.
Uteuzi huo mwendelezo wa waamuzi hao kuwakilisha Tanzania katika mashindano ya kimataifa yanayosimamiwa na CAF.
ADVERTISE HERE