Simba SC yafanya comeback ya kibabe, yaichapa Namungo mabao 3-2 Uhuru

Xtra 90 Media By Xtra 90 Media
•
2h ago
Simba SC yafanya comeback ya kibabe, yaichapa Namungo mabao 3-2 Uhuru

Simba SC imepata ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Namungo FC katika mchezo wa NBC Premier League uliopigwa kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam, baada ya kuonyesha uwezo mkubwa wa kurejea mchezoni kufuatia kuwa nyuma kwa mabao 2-1.

Anicet Oura aliipa Simba bao la mapema dakika ya 4, lakini Raymond Lulendi aliibadilishia Namungo matokeo kwa kufunga mabao mawili dakika ya 36 na 43, na kuifanya timu hiyo kwenda mapumziko ikiwa mbele kwa mabao 2-1.

Kipindi cha pili Simba ilirejea kwa nguvu kusaka matokeo, huku beki Rushine De Reuck akisawazisha kwa mkwaju wa penalti dakika ya 80 na kuamsha matumaini ya mashabiki wa Wekundu wa Msimbazi.

Dakika ya 89, Anicet Oura alifunga bao lake la pili katika mchezo huo na kukamilisha comeback ya Simba, ikiibuka na ushindi wa mabao 3-2.

Pongezi pia kwa Ibrahim Doumbia, ambaye aliingia akitokea benchi na kuathiri mchezo moja kwa moja baada ya kusababisha penalti iliyoisaidia Simba kurejea mchezoni.

Simba SC yaonyesha tabia ya kupambana hadi dakika za mwisho na kuondoka na pointi tatu muhimu.

ADVERTISE HERE

More Stories

Highlights : Simba 3-2 Namungo Fc, Ligi Kuu
Highlights : Simba 3-2 Namungo Fc, Ligi Kuu
3h ago
READ MORE →
Ratiba ya NBC Premier League leo, Simba dimbani kusaka alama tatu
Ratiba ya NBC Premier League leo, Simba dimbani kusaka alama tatu
12h ago
READ MORE →
Premier League yaomba radhi Chelsea kuhusu bao la Estêvão lililokataliwa dhidi ya Manchester United
Premier League yaomba radhi Chelsea kuhusu bao la Estêvão lililokataliwa dhidi ya Manchester United
15h ago
READ MORE →
Messi awasha moto, aiwezesha Inter Miami kufanya comeback dhidi ya New England Revolution
Messi awasha moto, aiwezesha Inter Miami kufanya comeback dhidi ya New England Revolution
15h ago
READ MORE →
Arsenal yaandika historia Anfield, yaichapa Liverpool na kuimarisha uongozi kileleni
Arsenal yaandika historia Anfield, yaichapa Liverpool na kuimarisha uongozi kileleni
1d ago
READ MORE →
Yanga yaiadhibu Kagera Sugar, yaibuka na ushindi mnono wa mabao 4-0
Yanga yaiadhibu Kagera Sugar, yaibuka na ushindi mnono wa mabao 4-0
1d ago
READ MORE →
Highlights : Yanga 4-0 Kagera Sugar, Ligi Kuu
Highlights : Yanga 4-0 Kagera Sugar, Ligi Kuu
1d ago
READ MORE →
Mnyama Simba SC yazindua jezi mpya kwa ajili ya CAF Champions League 2026/27
Mnyama Simba SC yazindua jezi mpya kwa ajili ya CAF Champions League 2026/27
1d ago
READ MORE →
TFF kusimamia uchaguzi wa Simba, ratiba kuboreshwa
TFF kusimamia uchaguzi wa Simba, ratiba kuboreshwa
1d ago
READ MORE →
Matola: Namungo ni timu imara, tunataka kutetea rekodi yetu
Matola: Namungo ni timu imara, tunataka kutetea rekodi yetu
1d ago
READ MORE →