Manchester United imeendelea kupitia kipindi kigumu baada ya kupoteza kwa mabao 2-0 dhidi ya Chelsea katika mchezo wa Ligi Kuu England uliopigwa Stamford Bridge siku ya Halloween.
Mabao ya Chelsea yalifungwa na Rogers pamoja na Cole Palmer, yakitosha kuipa timu hiyo ushindi muhimu mbele ya mashabiki wake.
Matokeo hayo yanaifanya Manchester United kupata kipigo cha tatu mfululizo katika mashindano yote, huku ikiendelea kusubiri ushindi mwingine kwenye Ligi Kuu England tangu Agosti 30, ambao ndio ushindi wake pekee wa ligi hadi sasa.
Hali ya United inazidi kuwa mbaya kwenye msimamo wa ligi, ikiwa pointi moja pekee juu ya eneo la kushuka daraja licha ya kuwa imecheza mchezo mmoja zaidi.
Kipigo hicho kinaongeza presha kwa Manchester United, ambayo inaendelea kukabiliwa na mwanzo mgumu wa msimu huu.