Mwenyekiti wa Simba SC, Murtaza Mangungu, amesema klabu hiyo hivi karibuni inatajia kumtamgaza CEO wake ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa katiba ya Simba inayohitaji timu hiyo kuwa na mtendaji wake mkuu ( CEO ).
Akizungumza na waandishi wa habari katika mkutano rasmi Mangungu amesema mchakato wa kumpata kiongozi mpya unaendelea, ingawa hakutaja jina la mgombea wala tarehe kamili ya kutangazwa kwake.
Nafasi ya CEO ni muhimu katika uendeshaji wa klabu, ikihusisha usimamizi wa shughuli za kibiashara, masoko na utekelezaji wa mipango ya taasisi nje ya uwanja. Simba imekuwa na mabadiliko katika nafasi hiyo katika miaka ya karibuni, ambapo Barbara Gonzalez akiwa ni miongoni mwa watendaji waliopita hivi karibuni ndani ya timu hiyo.
Kwa sasa, macho ya mashabiki wa Simba yanaelekezwa kwa uongozi wa klabu kusubiri tangazo la jina jipya.