Ligi Kuu ya NBC inaendelea leo raundi ya 9 ambapo mechi nne zinatarajiwa kupigwa katika viwanja mbalimbali.
Vinara wa ligi hiyo Simba wako ugenini mkoani Manyara kuikabili Foutain Gate kwenye mchezo utakaopigwa uwanja wa Tanzanite Kwaraa.
Simba inapewa nafasi kubwa ya kushinda mchezo huo na kuendelea kujiimarisha kileleni mwa msimamo wa ligi.
Mapema saa 8 mchana, Pamba Jiji itaikaribisha Singida BS katika mchezo utakaopigwa uwanja wa CCM Kirumba.
Mechi nyingine ni kati ya TRA United dhidi ya Geita Gold saa 10:15 jioni na kuhitimishwa na mchezo kati ya Namungo dhidi ya Polisi Tanzania, saa 1 usiku.

ADVERTISE HERE