Simba yatangaza tarehe ya mkutano mkuu na uchaguzi wa viongozi

Xtra 90 Media By Xtra 90 Media
β€’
23h ago
Simba yatangaza tarehe ya mkutano mkuu na uchaguzi wa viongozi

Bodi ya Wakurugenzi ya Klabu ya Simba SC imetangaza kuwa Mkutano Mkuu wa Kawaida wa Mwaka 2026 pamoja na uchaguzi wa viongozi wa klabu hiyo utafanyika Januari 3, 2027 jijini Dar es Salaam.

Kupitia taarifa iliyotolewa Oktoba 26, 2026, bodi hiyo imeeleza kuwa hatua hiyo inafanyika kwa mujibu wa Katiba ya Simba ya mwaka 2018, toleo la mwaka 2026.

Aidha, bodi imewataarifu wanachama wote kuwa wito rasmi wa mkutano, ajenda pamoja na nyaraka nyingine zinazohusiana na mkutano huo zitawasilishwa kwa wanachama kupitia matawi yao.

Bodi ya Wakurugenzi imewataka wanachama wa Simba kujiandaa kuhudhuria mkutano huo, ambao pamoja na masuala mengine utahusisha uchaguzi wa viongozi wa klabu hiyo.

Taarifa hiyo imehitimishwa kwa kusisitiza umuhimu wa wanachama kufuatilia mawasiliano rasmi kupitia matawi yao ili kupata maelezo zaidi kuhusu maandalizi ya mkutano na uchaguzi huo.

ADVERTISE HERE

More Stories

Alama tatu zabaki Jangwani, Yanga yaichapa Mashujaa FC
Alama tatu zabaki Jangwani, Yanga yaichapa Mashujaa FC
1h ago
READ MORE β†’
Highlights : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, Ligi Kuu
Highlights : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, Ligi Kuu
1h ago
READ MORE β†’
Simba yashusha Mkurugenzi wa Ufundi
Simba yashusha Mkurugenzi wa Ufundi
5h ago
READ MORE β†’
TFF yakutana na Simba, Yanga, Azam FC na Singida Black Stars kupanga mikakati ya michuano ya CAF
TFF yakutana na Simba, Yanga, Azam FC na Singida Black Stars kupanga mikakati ya michuano ya CAF
6h ago
READ MORE β†’
Lameck Kanyonga ataka magolikipa wazawa kupewa nafasi ya kuaminiwa
Lameck Kanyonga ataka magolikipa wazawa kupewa nafasi ya kuaminiwa
8h ago
READ MORE β†’
Tumefanyia kazi mapungufu yetu kuelekea mchezo dhidi ya Azam FC- Mayanga
Tumefanyia kazi mapungufu yetu kuelekea mchezo dhidi ya Azam FC- Mayanga
8h ago
READ MORE β†’
Ibenge ataka Azam FC kucheza kwa moyo na kutumia akili dhidi ya Mbeya City
Ibenge ataka Azam FC kucheza kwa moyo na kutumia akili dhidi ya Mbeya City
8h ago
READ MORE β†’
Michael Carrick aonekana Carrington huku Manchester United ikikabiliwa na presha
Michael Carrick aonekana Carrington huku Manchester United ikikabiliwa na presha
10h ago
READ MORE β†’
NBC Premier League kuendelea leo kwa michezo miwili
NBC Premier League kuendelea leo kwa michezo miwili
10h ago
READ MORE β†’
Washindi wa tuzo za Ballon d’Or kwa mwaka 2026.
Washindi wa tuzo za Ballon d’Or kwa mwaka 2026.
20h ago
READ MORE β†’