UEFA Champions League yashuhudia mabao mengi huku Manchester City na Roma zikifanya vizuri

Xtra 90 Media By Xtra 90 Media
β€’
4h ago
UEFA Champions League yashuhudia mabao mengi huku Manchester City na Roma zikifanya vizuri

Mashindano ya UEFA Champions League yameendelea kwa michezo yenye ushindani mkubwa na mabao mengi, huku Manchester City, AS Roma na Paris Saint Germain zikipata ushindi mnono katika michezo yao. Liverpool na Napoli pia zilipata ushindi katika michezo iliyokuwa na idadi kubwa ya mabao.

Katika mchezo wa saa 19:45, Fenerbahce ilitoka sare ya mabao mawili kwa mawili dhidi ya Slavia Prague. Fenerbahce ilianza kwa kasi kupitia Aydin aliyefunga dakika ya nne, kabla ya Greenwood kuongeza bao la pili dakika ya 11. Slavia Prague ilisawazisha kupitia Lukas Provod dakika ya 15 na Pavel Kacor dakika ya 90 na kufanya mchezo huo kumalizika kwa sare ya 2-2.Borussia Dortmund iliifunga Sabah mabao mawili kwa moja. Dortmund ilipata bao la kwanza kupitia Guirassy dakika ya 10, kabla ya Aden McCarthy kuisawazishia Sabah dakika ya 39. Guirassy alifunga bao lake la pili dakika ya 53 na kuipa Dortmund ushindi wa 2-1.Katika mchezo wa saa 22:00, FC Porto ilikubali kipigo cha bao moja kwa sifuri kutoka kwa PSV Eindhoven. Bao pekee la mchezo huo lilifungwa na Guus Til dakika ya 57 na kuipa PSV ushindi huo.Liverpool ilipata ushindi wa mabao manne kwa matatu dhidi ya Villarreal katika mchezo uliokuwa na ushindani mkubwa. Villarreal ilianza kwa bao la Mikautadze dakika ya nne, kabla ya Sergi Cardona kuongeza la pili dakika ya 29. Liverpool ilipunguza pengo kupitia Mac Allister dakika ya 36, kisha Araujo akaongeza bao la kusawazisha dakika ya 45 na 2. Mac Allister alifunga tena dakika ya 65 na Wirtz akaongeza bao la nne dakika ya 69. Villarreal ilipata bao la tatu kupitia Tani Oluwaseyi dakika ya 87, lakini Liverpool ikaondoka na ushindi wa 4-3.Manchester City iliichapa AEK Athens mabao matano kwa moja. Elliot Anderson alifungua ukurasa wa mabao dakika ya 12, kabla ya Foden kuongeza la pili dakika ya 34. AEK Athens ilipata bao lake kupitia Stavros Pilios dakika ya 52. Hata hivyo, Cherki aliiongezea City bao la tatu dakika ya 57, kabla ya Foden kufunga mara mbili zaidi dakika ya 65 na 76 na kukamilisha hat trick yake.Paris Saint Germain iliifunga Barcelona mabao manne kwa mawili katika mchezo uliokuwa ukisubiriwa kwa hamu. Desire Doue aliifungia PSG dakika ya 36 na kuifanya timu hiyo kwenda mapumziko ikiwa mbele kwa bao moja. Barcelona ilisawazisha kupitia Xavi Espart dakika ya 55, lakini Lucas Hernandez aliirudisha PSG mbele kwa kichwa dakika ya 72. Lamine Yamal alisawazisha tena kwa bao maridadi dakika ya 79, kabla ya Vitinha kufunga dakika ya 81 na Fabian Ruiz kuongeza bao la nne dakika ya 86 kwa pasi ya Achraf Hakimi.AS Roma iliifunga Slovan Bratislava mabao manne kwa sifuri. Hermoso alifungua ukurasa wa mabao dakika ya 21, kabla ya Molina kuongeza la pili dakika ya 39. Pisilli alifunga bao la tatu dakika ya 52 na Malen akakamilisha ushindi huo kwa mkwaju wa penalti dakika ya 58.Napoli ilipata ushindi wa mabao manne kwa matatu dhidi ya Bodo Glimt katika mchezo mwingine uliokuwa na mabao mengi. Politano aliifungia Napoli dakika ya kwanza, kabla ya Jens Hauge kuisawazishia Bodo Glimt dakika ya 27. McTominay aliirudisha Napoli mbele dakika ya 41 na kuongeza bao jingine dakika ya 75. Andreas Helmersen aliifungia Bodo Glimt dakika ya 62, huku bao la kujifunga la Odin Bjortuft dakika ya 88 likiipa Napoli bao la nne. Sondre Brunstad Fet alifunga bao la tatu la Bodo Glimt dakika ya 90 na 4, lakini Napoli ikaibuka na ushindi wa 4-3.Katika mchezo mwingine, Stuttgart na Atletico Madrid zilitoka sare ya bao moja kwa moja. Jamie Leweling aliifungia Stuttgart dakika ya 36, kabla ya Julian Alvarez kusawazishia Atletico Madrid dakika ya 47 na kufanya mchezo huo kumalizika kwa sare ya 1-1.

ADVERTISE HERE

More Stories

Mashabiki kesho ruksa kuitazama Simba na 15 de Agosto
Mashabiki kesho ruksa kuitazama Simba na 15 de Agosto
15h ago
READ MORE β†’
Petro de Luanda yamfuta kazi Pedro Sousa baada ya kipigo ligi ya mabingwa Afrika
Petro de Luanda yamfuta kazi Pedro Sousa baada ya kipigo ligi ya mabingwa Afrika
16h ago
READ MORE β†’
Prince Dube aikana Simba, aitaja Yanga kuwa timu yake ya moyoni
Prince Dube aikana Simba, aitaja Yanga kuwa timu yake ya moyoni
16h ago
READ MORE β†’
UEFA Champions League kuendelea leo, macho kuelekezwa PSG dhidi ya Barcelona
UEFA Champions League kuendelea leo, macho kuelekezwa PSG dhidi ya Barcelona
17h ago
READ MORE β†’
CAF yabadilisha mwamuzi wa mchezo wa Simba SC dhidi ya 15 de Agosto
CAF yabadilisha mwamuzi wa mchezo wa Simba SC dhidi ya 15 de Agosto
1d ago
READ MORE β†’
Kocha wa Wiliete SC alazwa hospitalini baada ya mchezo dhidi ya Mamelodi Sundowns
Kocha wa Wiliete SC alazwa hospitalini baada ya mchezo dhidi ya Mamelodi Sundowns
1d ago
READ MORE β†’
TFF kuja na zoezi la upimaji wa dawa zilizokatazwa kwa wachezaji
TFF kuja na zoezi la upimaji wa dawa zilizokatazwa kwa wachezaji
1d ago
READ MORE β†’
Azam FC yawasha moto, yaanza maandalizi kuivunja ZED FC Chamazi
Azam FC yawasha moto, yaanza maandalizi kuivunja ZED FC Chamazi
1d ago
READ MORE β†’
Simba kuweka big screen Mwembe Yanga, mashabiki watakiwa kuvaa jezi mpya
Simba kuweka big screen Mwembe Yanga, mashabiki watakiwa kuvaa jezi mpya
1d ago
READ MORE β†’
Rangers yaelekea Caf kufuatia vurugu za mashabiki wa Mc Alger
Rangers yaelekea Caf kufuatia vurugu za mashabiki wa Mc Alger
1d ago
READ MORE β†’