Simba baada ya kuigaragaza Yanga, kituo kinachofuata ni Mashujaa Fc

Joel JJ By Joel JJ
•
2h ago
Simba baada ya kuigaragaza Yanga, kituo kinachofuata ni Mashujaa Fc

Kikosi cha Simba SC kinarejea dimbani Jumanne kukabiliana na Mashujaa FC katika mwendelezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara, kikitoka kupata ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya watani wao wa jadi, Yanga SC.

Mchezo huo wa watani wa jadi ulipigwa juzi kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam, ambapo Simba iliibuka na ushindi muhimu na kuendeleza mwenendo wake mzuri katika ligi msimu huu.

Baada ya ushindi huo, Wekundu wa Msimbazi sasa wanaelekeza nguvu zao kwenye mchezo dhidi ya Mashujaa FC, unaotarajiwa kuchezwa kwenye Uwanja wa Isamuhyo jijini Dar es Salaam.

Kocha Mkuu wa Simba, Steve Barker, ameweka wazi kuwa kikosi chake kimehitimisha shangwe za ushindi dhidi ya Yanga na sasa kimejikita kikamilifu katika maandalizi ya mchezo unaofuata.

Barker analenga kuendeleza rekodi yake ya ushindi wa asilimia 100 tangu aanze kampeni za ligi msimu huu, huku Simba ikiwa imeshinda michezo yote saba ya mwanzo na kukusanya alama 21, matokeo yanayoifanya kukaa kileleni mwa msimamo wa ligi.

Simba Kuelekeza Nguvu Ligi ya Mabingwa Afrika

Baada ya kumaliza mchezo dhidi ya Mashujaa FC, Simba itageukia mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika, ambako inapambana kufuzu hatua ya makundi.

Wekundu wa Msimbazi wataanza safari hiyo kwa kucheza ugenini dhidi ya 15 de Agosto ya Guinea ya Ikweta Oktoba 17 au 18, kabla ya kurejea jijini Dar es Salaam kwa mchezo wa marudiano.

ADVERTISE HERE

More Stories

Ahmed Ally na Haji Manara wamtetea Mngqithi baada ya kipigo cha dabi
Ahmed Ally na Haji Manara wamtetea Mngqithi baada ya kipigo cha dabi
45m ago
READ MORE →
Ahmed Ally asifia ubora wa Diarra, akumbusha nafasi alizookoa dhidi ya Simba
Ahmed Ally asifia ubora wa Diarra, akumbusha nafasi alizookoa dhidi ya Simba
1h ago
READ MORE →
Coastal Union kuikaribisha Singida BS ligi kuu NBC leo
Coastal Union kuikaribisha Singida BS ligi kuu NBC leo
2h ago
READ MORE →
TRA United vs Yanga wasogezwa mbele, kupigwa Oktoba 24
TRA United vs Yanga wasogezwa mbele, kupigwa Oktoba 24
3h ago
READ MORE →
Manchester City yaichapa Liverpool 3-0, Anderson aibuka mchezaji bora.
Manchester City yaichapa Liverpool 3-0, Anderson aibuka mchezaji bora.
14h ago
READ MORE →
Carrick kupewa mechi mbili kuokoa kibarua chake Manchester United.
Carrick kupewa mechi mbili kuokoa kibarua chake Manchester United.
16h ago
READ MORE →
EPL: Mechi za leo, Liverpool na Manchester City Kusaka mbabe
EPL: Mechi za leo, Liverpool na Manchester City Kusaka mbabe
23h ago
READ MORE →
Manqoba amtaja Abuya kipigo dhidi ya Simba
Manqoba amtaja Abuya kipigo dhidi ya Simba
1d ago
READ MORE →
Barcelona inagawa dozi tu La Liga, yaipiga Getafe 3-0
Barcelona inagawa dozi tu La Liga, yaipiga Getafe 3-0
1d ago
READ MORE →
Real Madrid yaishinda kwa tabu Villarreal, Vinícius Jr apewa kadi nyekundu
Real Madrid yaishinda kwa tabu Villarreal, Vinícius Jr apewa kadi nyekundu
1d ago
READ MORE →