JKT Tanzania imeibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Fountain Gate katika mchezo wa NBC Premier League uliomalizika hivi punde.
Fountain Gate ndiyo iliyokuwa ya kwanza kupata bao kupitia Sadick Ramadhan, aliyefunga dakika ya 55 na kuipa timu yake matumaini ya kuondoka na ushindi katika mchezo huo.
Hata hivyo, JKT Tanzania ilisawazisha kupitia Karim Mfaume dakika ya 86, kabla ya Salum Khamis kufunga bao la ushindi dakika ya 90+2 na kuipa JKT Tanzania pointi zote tatu.
Matokeo hayo yanaifanya JKT Tanzania kuondoka na ushindi muhimu katika mchezo uliokuwa na ushindani hadi dakika za mwisho.
ADVERTISE HERE