Beno Ngassa na Fikiri Elias wang'ara tuzo za Peptemba

Abdulrahman Said By Abdulrahman Said
β€’
2h ago
Beno Ngassa na Fikiri Elias wang'ara tuzo za Peptemba

Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) imetangaza washindi wa Tuzo za Mwezi Septemba kwa Ligi Kuu ya NBC msimu wa 2026/27, huku mshambuliaji wa Dodoma Jiji, Berno Ngassa, akichaguliwa Mchezaji Bora wa Mwezi na Fikiri Elias wa Coastal Union akitwaa tuzo ya Kocha Bora.

Ngassa amefanikiwa kuibuka mshindi mbele ya Maabad Maabad wa Coastal Union na Anuary Jabir wa Polisi Tanzania, baada ya kuonyesha kiwango bora katika michezo miwili ambayo Dodoma Jiji ilicheza mwezi huo. Timu hiyo ilishinda michezo yote miwili, huku Ngassa akifunga bao moja na kuhusika katika bao jingine.

Kwa upande wa makocha, Fikiri Elias amewaacha nyuma Steve Barker wa Simba na Vincent Mashami wa Dodoma Jiji. Kocha huyo aliiongoza Coastal Union kushinda michezo yote miwili ya Septemba, matokeo yaliyosaidia timu hiyo kupanda kutoka nafasi ya 15 hadi ya 11 katika msimamo wa ligi.

TPLB pia imeteua mabao matatu yanayowania Tuzo ya Bao Bora la Mwezi Septemba, ambayo yataamuliwa kwa kura za mashabiki. Mabao hayo ni ya Haroun Lyawatwa wa Mashujaa dhidi ya Singida Black Stars, Anuary Jabir wa Polisi Tanzania dhidi ya Mbeya City na Mohamed Damaro wa Singida Black Stars dhidi ya Namungo.

Katika NBC Championship, Ramadhan Kalanje wa KMC ametwaa Tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwezi Septemba, akiwashinda Abiud Mtambuku wa Mbeya Kwanza na kipa Haroun Mandanda wa Rhino Rangers. Kwa upande wa makocha, Mohamed Muya wa KMC amechaguliwa Kocha Bora baada ya kuiongoza timu yake kushinda michezo yote mitatu iliyocheza mwezi huo.

Β 

ADVERTISE HERE

More Stories

Pedro astaafu soka baada ya safari yenye mafanikio.
Pedro astaafu soka baada ya safari yenye mafanikio.
3m ago
READ MORE β†’
Ahmed Ally: Steve Barker haioni Simba kama mnyonge mbele ya Yanga
Ahmed Ally: Steve Barker haioni Simba kama mnyonge mbele ya Yanga
41m ago
READ MORE β†’
Arteta yupo sana London, asaini mkataba mpya na Arsenal hadi 2030
Arteta yupo sana London, asaini mkataba mpya na Arsenal hadi 2030
1h ago
READ MORE β†’
Dabi ya Cairo yawadia Zamalek kukabiliana na Al ahly oktoba 11
Dabi ya Cairo yawadia Zamalek kukabiliana na Al ahly oktoba 11
3h ago
READ MORE β†’
Simba yatangaza viingilio vya dabi ya kariakoo dhidi ya Yanga
Simba yatangaza viingilio vya dabi ya kariakoo dhidi ya Yanga
4h ago
READ MORE β†’
TFF yamwamuru Mwenda kurejea Yanga na kuheshimu mkataba
TFF yamwamuru Mwenda kurejea Yanga na kuheshimu mkataba
16h ago
READ MORE β†’
Ronaldo afafanua sababu za kuondoka kambini Portugal.
Ronaldo afafanua sababu za kuondoka kambini Portugal.
17h ago
READ MORE β†’
Ronaldo afichua kilichotokea kati yake na Jorge Jesus
Ronaldo afichua kilichotokea kati yake na Jorge Jesus
17h ago
READ MORE β†’
Messi atunukiwa shahada ya heshima na Chuo Kikuu cha Buenos Aires.
Messi atunukiwa shahada ya heshima na Chuo Kikuu cha Buenos Aires.
17h ago
READ MORE β†’
Stars U23 yakwama mbele ya Kenya kufuzu Afcon
Stars U23 yakwama mbele ya Kenya kufuzu Afcon
21h ago
READ MORE β†’