Kuelekea Derby ya Kariakoo ya Oktoba 10, kocha wa Simba SC, Steve Barker, ameweka wazi kuwa mchezo dhidi ya Yanga hautakuwa wa kawaida, akitambua ugumu na uzito wa pambano hilo.
Lakini nyuma ya kauli yake kuna jambo jingine linalovutia zaidi: Simba inalenga kutumia derby hiyo kuendeleza mfululizo wake wa ushindi hadi kufikisha mechi saba mfululizo.
Barker amesema maandalizi ya timu yamejikita katika kuhakikisha Simba inaingia kwenye mchezo huo ikiwa tayari kupambana kwa dakika zote.
Β βMchezo wa tarehe 10 dhidi ya Yanga najua utakuwa mzuri, lakini pia mgumu. Sisi kama Simba tumejipanga kuhakikisha tunashinda ili tuwe tumeshinda michezo saba mfululizo.β
Kambi ya Afrika Kusini imewapa nini? Simba imeweka sehemu ya maandalizi yake nchini Afrika Kusini, na Barker anaamini kambi hiyo imeongeza kitu muhimu ndani ya kikosi kujiamini.Β
βKambi ya hapa Afrika Kusini kuna kitu imetuongezea, naamini tutakwenda kupambana siku hiyo tupate ushindi.β
Sasa swali kubwa linabaki kwenye uwanja: Je, maandalizi ya Afrika Kusini na kasi ya ushindi wa Simba vitatosha kuipa timu hiyo ushindi dhidi ya Yanga?