Spain yaichapa England 3-2 Wembley.

Xtra 90 Media By Xtra 90 Media
β€’
26 Sep 2026
Spain yaichapa England 3-2 Wembley.

Mabingwa wa dunia, Spain, wameanza kampeni yao mpya ya Nations League kwa ushindi wa kuvutia baada ya kuifunga England mabao 3-2 katika mchezo uliopigwa kwenye dimba la Wembley.

Spain ilianza mchezo kwa kasi na kufungua ukurasa wa mabao mapema kabisa dakika ya pili kupitia Lamine Yamal, aliyeipa timu yake uongozi wa 1-0.

England haikukaa chini na ilifanikiwa kugeuza matokeo kabla ya mapumziko. Anthony Gordon alisawazisha dakika ya 36, kabla ya Harry Kane kuifungia England bao la pili dakika ya 40 na kuwapeleka mapumziko wakiwa mbele kwa 2-1.

Kipindi cha pili kilikuwa cha Spain, ambayo ilionyesha ubora wake na kurejea mchezoni. Alex Baena alisawazisha dakika ya 60, akiifanya mechi kuwa 2-2.

Spain iliendelea kushambulia na juhudi zake zikazaa matunda dakika ya 74, pale Mikel Oyarzabal alipofunga bao la tatu na kuipa timu yake ushindi wa 3-2.

Matokeo hayo yanaipa Spain mwanzo mzuri wa kampeni yake mpya ya Nations League, huku England ikianza safari hiyo kwa kipigo mbele ya mashabiki wake Wembley.

ADVERTISE HERE

More Stories

Mashabiki kesho ruksa kuitazama Simba na 15 de Agosto
Mashabiki kesho ruksa kuitazama Simba na 15 de Agosto
2h ago
READ MORE β†’
Petro de Luanda yamfuta kazi Pedro Sousa baada ya kipigo ligi ya mabingwa Afrika
Petro de Luanda yamfuta kazi Pedro Sousa baada ya kipigo ligi ya mabingwa Afrika
3h ago
READ MORE β†’
Prince Dube aikana Simba, aitaja Yanga kuwa timu yake ya moyoni
Prince Dube aikana Simba, aitaja Yanga kuwa timu yake ya moyoni
3h ago
READ MORE β†’
UEFA Champions League kuendelea leo, macho kuelekezwa PSG dhidi ya Barcelona
UEFA Champions League kuendelea leo, macho kuelekezwa PSG dhidi ya Barcelona
4h ago
READ MORE β†’
CAF yabadilisha mwamuzi wa mchezo wa Simba SC dhidi ya 15 de Agosto
CAF yabadilisha mwamuzi wa mchezo wa Simba SC dhidi ya 15 de Agosto
1d ago
READ MORE β†’
Kocha wa Wiliete SC alazwa hospitalini baada ya mchezo dhidi ya Mamelodi Sundowns
Kocha wa Wiliete SC alazwa hospitalini baada ya mchezo dhidi ya Mamelodi Sundowns
1d ago
READ MORE β†’
TFF kuja na zoezi la upimaji wa dawa zilizokatazwa kwa wachezaji
TFF kuja na zoezi la upimaji wa dawa zilizokatazwa kwa wachezaji
1d ago
READ MORE β†’
Azam FC yawasha moto, yaanza maandalizi kuivunja ZED FC Chamazi
Azam FC yawasha moto, yaanza maandalizi kuivunja ZED FC Chamazi
1d ago
READ MORE β†’
Simba kuweka big screen Mwembe Yanga, mashabiki watakiwa kuvaa jezi mpya
Simba kuweka big screen Mwembe Yanga, mashabiki watakiwa kuvaa jezi mpya
1d ago
READ MORE β†’
Rangers yaelekea Caf kufuatia vurugu za mashabiki wa Mc Alger
Rangers yaelekea Caf kufuatia vurugu za mashabiki wa Mc Alger
1d ago
READ MORE β†’