Aziz Ki awaachia wanzake msala Kariakoo Derby

Joel JJ By Joel JJ
•
23 Sep 2026
Aziz Ki awaachia wanzake msala Kariakoo Derby

Nyota wa Yanga, Stephane Aziz Ki, amewaachia wachezaji wenzake ‘msala’ wa kuhakikisha wanafanya kazi hiyo katika Dabi ya Kariakoo dhidi ya Simba, baada ya yeye kuthibitishwa kuwa hatakuwa sehemu ya kikosi kitakachokutana na watani hao wa jadi Oktoba 10.

Aziz Ki atalazimika kuikosa dabi hiyo baada ya kuonyeshwa kadi nyekundu katika mchezo dhidi ya Geita Gold, kufuatia tukio lililomhusisha mchezaji wa timu hiyo, Datius Peter.

Kadi hiyo imemfanya kiungo huyo kutumikia adhabu ya michezo miwili, huku mchezo wa kwanza akiwa ni dhidi ya Simba na baadaye kuukosa pia mchezo dhidi ya TRA United.

Awali, Yanga iliwasilisha malalamiko kwa Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB), ikiomba kadi hiyo ifutwe kwa madai kuwa Aziz Ki hakukusudia kumuumiza Datius Peter.

Hata hivyo, baada ya kutolewa kwa taarifa ya Kamati ya Saa 72, hakuna kilichobadilika na sasa mchezaji huyo atalazimika kutumikia adhabu hiyo.

Licha ya kutokuwepo katika mchezo ambao una uzito mkubwa kwa mashabiki wa pande zote mbili, Aziz Ki amesema hana hofu na uwezo wa kikosi cha Yanga, akisisitiza kuwa timu hiyo haimtegemei mchezaji mmoja.

“Ninaamini kwenye kikosi chetu. Yanga ina wachezaji wengi wazuri na kila mmoja ana uwezo wa kuisaidia timu. Mimi sitakuwepo, lakini naamini wenzangu watafanya kazi nzuri,” alisema Aziz Ki.

Kiungo huyo mwenye uzoefu wa kucheza Kariakoo Derby amesema anatamani angekuwa uwanjani kusaidia timu, lakini kutokana na adhabu hiyo, jukumu lake litakuwa kuwaunga mkono wachezaji wenzake akiwa nje ya uwanja.

“Nitakuwa pamoja nao kwa moyo. Natamani ningekuwa uwanjani kusaidia timu, lakini kwa kuwa sitakuwepo, nitawaunga mkono na kuamini watafanya vizuri,” alisema.

Aziz Ki amekuwa miongoni mwa wachezaji muhimu wa Yanga katika misimu ya nyuma, huku uwepo wake katika michezo dhidi ya Simba ukiwa umeacha kumbukumbu kadhaa kwa mashabiki wa Yanga.

Sasa, kwa kutokuwepo kwake katika Dabi ya Oktoba 10, jukumu la kuziba pengo lake litakuwa kwa wachezaji wengine wa Yanga ambao watapewa nafasi katika mchezo huo unaotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa.

ADVERTISE HERE

More Stories

Mashabiki kesho ruksa kuitazama Simba na 15 de Agosto
Mashabiki kesho ruksa kuitazama Simba na 15 de Agosto
49m ago
READ MORE →
Petro de Luanda yamfuta kazi Pedro Sousa baada ya kipigo ligi ya mabingwa Afrika
Petro de Luanda yamfuta kazi Pedro Sousa baada ya kipigo ligi ya mabingwa Afrika
1h ago
READ MORE →
Prince Dube aikana Simba, aitaja Yanga kuwa timu yake ya moyoni
Prince Dube aikana Simba, aitaja Yanga kuwa timu yake ya moyoni
1h ago
READ MORE →
UEFA Champions League kuendelea leo, macho kuelekezwa PSG dhidi ya Barcelona
UEFA Champions League kuendelea leo, macho kuelekezwa PSG dhidi ya Barcelona
2h ago
READ MORE →
CAF yabadilisha mwamuzi wa mchezo wa Simba SC dhidi ya 15 de Agosto
CAF yabadilisha mwamuzi wa mchezo wa Simba SC dhidi ya 15 de Agosto
1d ago
READ MORE →
Kocha wa Wiliete SC alazwa hospitalini baada ya mchezo dhidi ya Mamelodi Sundowns
Kocha wa Wiliete SC alazwa hospitalini baada ya mchezo dhidi ya Mamelodi Sundowns
1d ago
READ MORE →
TFF kuja na zoezi la upimaji wa dawa zilizokatazwa kwa wachezaji
TFF kuja na zoezi la upimaji wa dawa zilizokatazwa kwa wachezaji
1d ago
READ MORE →
Azam FC yawasha moto, yaanza maandalizi kuivunja ZED FC Chamazi
Azam FC yawasha moto, yaanza maandalizi kuivunja ZED FC Chamazi
1d ago
READ MORE →
Simba kuweka big screen Mwembe Yanga, mashabiki watakiwa kuvaa jezi mpya
Simba kuweka big screen Mwembe Yanga, mashabiki watakiwa kuvaa jezi mpya
1d ago
READ MORE →
Rangers yaelekea Caf kufuatia vurugu za mashabiki wa Mc Alger
Rangers yaelekea Caf kufuatia vurugu za mashabiki wa Mc Alger
1d ago
READ MORE →