Palmer, Rashford na Mainoo watajwa kujitoa kikosi cha Uingereza

Abdulrahman Said By Abdulrahman Said
β€’
21 Sep 2026
Palmer, Rashford na Mainoo watajwa kujitoa kikosi cha Uingereza

Cole Palmer, Marcus Rashford na Kobbie Mainoo wanatajwa kuwa miongoni mwa wachezaji wanaotarajiwa kujiondoa kwenye kikosi cha England kuelekea michezo ya UEFA Nations League, huku chanzo kikitajwa ni changamoto za majeraha na utimamu wa wachezaji hao. 

Palmer, ambaye alirejeshwa kwenye kikosi cha England baada ya kukosa Kombe la Dunia 2026, ameripotiwa kujiondoa kwa sababu zinazohusishwa na usimamizi wa mzigo wa michezo pamoja na tatizo dogo la misuli. Mshambuliaji huyo wa Chelsea amekuwa na mwanzo mzuri msimu huu, akifunga mabao manne na kutoa assists mbili katika mechi saba, kabla ya kucheza dakika zote 90 katika kipigo cha 3-0 dhidi ya Brentford.

Kwa upande wa Manchester United, Rashford anatarajiwa kufanyiwa tathmini kutokana na tatizo la nyonga ambalo limekuwa likishughulikiwa na klabu, baada ya kutolewa katika sare ya 1-1 dhidi ya Fulham. Mainoo naye anatajwa kuwa huenda akakosekana kutokana na tatizo la majeraha.

England iliwajumuisha wachezaji hao watatu kwenye kikosi cha watu 27 kilichotangazwa Septemba 18, lakini sasa huenda Tuchel akalazimika kufanya mabadiliko kabla ya kuanza kwa kampeni ya Nations League. England itaanza dhidi ya mabingwa wa dunia Hispania Septemba 26 katika Uwanja wa Wembley, kabla ya kukutana na Czechia na Croatia katika michezo inayofuata.

ADVERTISE HERE

More Stories

Mashabiki kesho ruksa kuitazama Simba na 15 de Agosto
Mashabiki kesho ruksa kuitazama Simba na 15 de Agosto
2h ago
READ MORE β†’
Petro de Luanda yamfuta kazi Pedro Sousa baada ya kipigo ligi ya mabingwa Afrika
Petro de Luanda yamfuta kazi Pedro Sousa baada ya kipigo ligi ya mabingwa Afrika
3h ago
READ MORE β†’
Prince Dube aikana Simba, aitaja Yanga kuwa timu yake ya moyoni
Prince Dube aikana Simba, aitaja Yanga kuwa timu yake ya moyoni
3h ago
READ MORE β†’
UEFA Champions League kuendelea leo, macho kuelekezwa PSG dhidi ya Barcelona
UEFA Champions League kuendelea leo, macho kuelekezwa PSG dhidi ya Barcelona
4h ago
READ MORE β†’
CAF yabadilisha mwamuzi wa mchezo wa Simba SC dhidi ya 15 de Agosto
CAF yabadilisha mwamuzi wa mchezo wa Simba SC dhidi ya 15 de Agosto
1d ago
READ MORE β†’
Kocha wa Wiliete SC alazwa hospitalini baada ya mchezo dhidi ya Mamelodi Sundowns
Kocha wa Wiliete SC alazwa hospitalini baada ya mchezo dhidi ya Mamelodi Sundowns
1d ago
READ MORE β†’
TFF kuja na zoezi la upimaji wa dawa zilizokatazwa kwa wachezaji
TFF kuja na zoezi la upimaji wa dawa zilizokatazwa kwa wachezaji
1d ago
READ MORE β†’
Azam FC yawasha moto, yaanza maandalizi kuivunja ZED FC Chamazi
Azam FC yawasha moto, yaanza maandalizi kuivunja ZED FC Chamazi
1d ago
READ MORE β†’
Simba kuweka big screen Mwembe Yanga, mashabiki watakiwa kuvaa jezi mpya
Simba kuweka big screen Mwembe Yanga, mashabiki watakiwa kuvaa jezi mpya
1d ago
READ MORE β†’
Rangers yaelekea Caf kufuatia vurugu za mashabiki wa Mc Alger
Rangers yaelekea Caf kufuatia vurugu za mashabiki wa Mc Alger
1d ago
READ MORE β†’