Afcon haiwezi kuondoka Tanzania, Kenya na Uganda : Motsepe

Abdulrahman Said By Abdulrahman Said
β€’
17 Sep 2026
Afcon haiwezi kuondoka Tanzania, Kenya na Uganda : Motsepe

Rais wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF), Dkt. Patrice Motsepe, amesisitiza kuwa Tanzania, Kenya na Uganda wataendelea kuwa wenyeji wa Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2027, akipuuza taarifa zinazodai kuwa mashindano hayo yanaweza kuhamishiwa nchi nyingine.

Motsepe ametoa msimamo huo Septemba 17, 2026, wakati wa ziara yake nchini Tanzania iliyolenga kukagua maendeleo ya maandalizi ya AFCON 2027. Ziara hiyo imejumuisha ukaguzi wa Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam pamoja na mkutano na Serikali ya Tanzania kuhusu maandalizi ya mashindano hayo. CAF ilikuwa imetangaza mapema kuwa ziara hiyo inalenga kutathmini maendeleo, kubaini maeneo yanayohitaji maboresho na kuhakikisha maandalizi yanaendana na mahitaji ya mashindano.

AFCON 2027 itakuwa mashindano ya kwanza katika historia kuandaliwa kwa pamoja na nchi tatu, Tanzania, Kenya na Uganda. CAF imethibitisha kuwa mashindano hayo yataanza Juni 19 na kumalizika Julai 17, 2027, huku nchi hizo tatu zikiwa zimefuzu moja kwa moja kama wenyeji.

Ziara ya Motsepe nchini Tanzania inafanyika wakati maandalizi yakiingia hatua muhimu, baada ya ujumbe wa CAF kufanya ukaguzi wa miundombinu katika nchi zote tatu mapema Septemba. Baada ya Tanzania, Motsepe anatarajiwa kuelekea Kenya kwa ajili ya kukutana na Serikali na kukagua miundombinu itakayotumika katika AFCON 2027.

ADVERTISE HERE

More Stories

Mashabiki kesho ruksa kuitazama Simba na 15 de Agosto
Mashabiki kesho ruksa kuitazama Simba na 15 de Agosto
1h ago
READ MORE β†’
Petro de Luanda yamfuta kazi Pedro Sousa baada ya kipigo ligi ya mabingwa Afrika
Petro de Luanda yamfuta kazi Pedro Sousa baada ya kipigo ligi ya mabingwa Afrika
2h ago
READ MORE β†’
Prince Dube aikana Simba, aitaja Yanga kuwa timu yake ya moyoni
Prince Dube aikana Simba, aitaja Yanga kuwa timu yake ya moyoni
2h ago
READ MORE β†’
UEFA Champions League kuendelea leo, macho kuelekezwa PSG dhidi ya Barcelona
UEFA Champions League kuendelea leo, macho kuelekezwa PSG dhidi ya Barcelona
3h ago
READ MORE β†’
CAF yabadilisha mwamuzi wa mchezo wa Simba SC dhidi ya 15 de Agosto
CAF yabadilisha mwamuzi wa mchezo wa Simba SC dhidi ya 15 de Agosto
1d ago
READ MORE β†’
Kocha wa Wiliete SC alazwa hospitalini baada ya mchezo dhidi ya Mamelodi Sundowns
Kocha wa Wiliete SC alazwa hospitalini baada ya mchezo dhidi ya Mamelodi Sundowns
1d ago
READ MORE β†’
TFF kuja na zoezi la upimaji wa dawa zilizokatazwa kwa wachezaji
TFF kuja na zoezi la upimaji wa dawa zilizokatazwa kwa wachezaji
1d ago
READ MORE β†’
Azam FC yawasha moto, yaanza maandalizi kuivunja ZED FC Chamazi
Azam FC yawasha moto, yaanza maandalizi kuivunja ZED FC Chamazi
1d ago
READ MORE β†’
Simba kuweka big screen Mwembe Yanga, mashabiki watakiwa kuvaa jezi mpya
Simba kuweka big screen Mwembe Yanga, mashabiki watakiwa kuvaa jezi mpya
1d ago
READ MORE β†’
Rangers yaelekea Caf kufuatia vurugu za mashabiki wa Mc Alger
Rangers yaelekea Caf kufuatia vurugu za mashabiki wa Mc Alger
1d ago
READ MORE β†’