Ngorongoro herous yalenga mwanzo wa ushindi dhidi ya Rwanda kuelekea Afcon U20

Abdulrahman Said By Abdulrahman Said
β€’
15 Sep 2026
Ngorongoro herous yalenga mwanzo wa ushindi dhidi ya Rwanda kuelekea Afcon U20

Timu ya Taifa ya Tanzania ya vijana chini ya miaka 20, Ngorongoro Heroes, leo Jumanne, Septemba 15, 2026, inashuka dimbani kuikabili Rwanda katika mchezo wa kwanza wa Kundi A wa michuano ya kuwania kufuzu AFCON U20 kwa ukanda wa CECAFA, mchezo utakaochezwa Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam, kuanzia saa 20:00.

Tanzania inaingia kwenye mchezo huo ikiwa mwenyeji wa mashindano hayo na pia bingwa mtetezi wa michuano ya CECAFA U20, huku Rwanda ikiwa miongoni mwa timu zinazowania nafasi ya kusonga mbele kutoka Kundi A linalojumuisha pia Ethiopia. Mfumo wa mashindano unaelekeza mshindi wa kila kundi pamoja na timu moja bora iliyomaliza nafasi ya pili kufuzu hatua ya nusu fainali.

Kwa upande wa Rwanda, kikosi hicho kimewasili Dar es Salaam kikiwa na maandalizi ya wiki kadhaa, huku kikiwa kimetoka kucheza michezo miwili ya kirafiki dhidi ya Sudan U20. Rwanda imeeleza kuwa iko tayari kwa changamoto hiyo dhidi ya wenyeji Tanzania katika mchezo huo wa ufunguzi.

Ngorongoro Heroes sasa inalenga kutumia faida ya kucheza nyumbani kuanza kampeni hiyo kwa ushindi na kuweka msingi mzuri wa kufuzu hatua inayofuata pamoja na kuwania tiketi ya kuiwakilisha CECAFA katika AFCON U20 2027 nchini Ghana.

ADVERTISE HERE

More Stories

Mashabiki kesho ruksa kuitazama Simba na 15 de Agosto
Mashabiki kesho ruksa kuitazama Simba na 15 de Agosto
2h ago
READ MORE β†’
Petro de Luanda yamfuta kazi Pedro Sousa baada ya kipigo ligi ya mabingwa Afrika
Petro de Luanda yamfuta kazi Pedro Sousa baada ya kipigo ligi ya mabingwa Afrika
3h ago
READ MORE β†’
Prince Dube aikana Simba, aitaja Yanga kuwa timu yake ya moyoni
Prince Dube aikana Simba, aitaja Yanga kuwa timu yake ya moyoni
3h ago
READ MORE β†’
UEFA Champions League kuendelea leo, macho kuelekezwa PSG dhidi ya Barcelona
UEFA Champions League kuendelea leo, macho kuelekezwa PSG dhidi ya Barcelona
4h ago
READ MORE β†’
CAF yabadilisha mwamuzi wa mchezo wa Simba SC dhidi ya 15 de Agosto
CAF yabadilisha mwamuzi wa mchezo wa Simba SC dhidi ya 15 de Agosto
1d ago
READ MORE β†’
Kocha wa Wiliete SC alazwa hospitalini baada ya mchezo dhidi ya Mamelodi Sundowns
Kocha wa Wiliete SC alazwa hospitalini baada ya mchezo dhidi ya Mamelodi Sundowns
1d ago
READ MORE β†’
TFF kuja na zoezi la upimaji wa dawa zilizokatazwa kwa wachezaji
TFF kuja na zoezi la upimaji wa dawa zilizokatazwa kwa wachezaji
1d ago
READ MORE β†’
Azam FC yawasha moto, yaanza maandalizi kuivunja ZED FC Chamazi
Azam FC yawasha moto, yaanza maandalizi kuivunja ZED FC Chamazi
1d ago
READ MORE β†’
Simba kuweka big screen Mwembe Yanga, mashabiki watakiwa kuvaa jezi mpya
Simba kuweka big screen Mwembe Yanga, mashabiki watakiwa kuvaa jezi mpya
1d ago
READ MORE β†’
Rangers yaelekea Caf kufuatia vurugu za mashabiki wa Mc Alger
Rangers yaelekea Caf kufuatia vurugu za mashabiki wa Mc Alger
1d ago
READ MORE β†’