Mwalimu ruksa kuitumikia Yanga, ITC yake yatumwa TFF

Joel JJ By Joel JJ
β€’
28 Aug 2026
Mwalimu ruksa kuitumikia Yanga, ITC yake yatumwa TFF

Huenda mashabiki wa Yanga leo wakapata nafasi ya kumshuhudia mshambuliaji wao mpya, Seleman Mwalimu, akicheza kwa mara ya kwanza katika kikosi hicho kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania dhidi ya Pamba Jiji.

Yanga itakuwa mwenyeji wa Pamba Jiji leo Ijumaa, Agosti 28, katika mchezo utakaopigwa saa 3:00 usiku kwenye Uwanja wa KMC Complex.

Mwalimu, ambaye usajili wake uliibua gumzo wakati wa dirisha la usajili baada ya Yanga kumnasa kutoka kwenye kambi ya watani wao, Simba SC, alikuwa hajaanza kuitumikia timu hiyo kutokana na kusubiriwa kwa hati yake ya kimataifa ya uhamisho wa mchezaji (ITC).

Hata hivyo, taarifa zinaeleza kuwa suala hilo sasa limepata ufumbuzi baada ya Shirikisho la Soka la Morocco (FRMF) kutuma ITC ya mshambuliaji huyo kwa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), hatua inayomuweka katika nafasi ya kuanza kuitumikia Yanga.

Iwapo kocha Manqoba Mngqithi ataamua kumtumia, Mwalimu anaweza kuonekana uwanjani leo dhidi ya Pamba Jiji, huku mashabiki wa Yanga wakisubiri kwa hamu kumuona mchezaji huyo mpya akianza safari yake rasmi katika klabu hiyo.

Tofauti na Stephane Aziz Ki, ambaye Mngqithi alisema bado hajawa tayari kucheza, Mwalimu anaonekana kuwa katika nafasi nzuri zaidi kwa kuwa amepata muda wa kutosha wa kufanya mazoezi na timu.

Kabla ya kusajiliwa na Yanga, Mwalimu alikuwa sehemu ya maandalizi ya msimu mpya katika kambi za Simba na Wydad Casablanca, hivyo tayari alikuwa katika programu za mazoezi ya kabla ya msimu (pre-season).

ADVERTISE HERE

More Stories

Coastal Union yaendeleza ubabe wa nyumbani, yaichapa Singida Black Stars
Coastal Union yaendeleza ubabe wa nyumbani, yaichapa Singida Black Stars
9h ago
READ MORE β†’
Simba SC yaendeleza ubabe, yabaki bila kipigo baada ya mechi saba
Simba SC yaendeleza ubabe, yabaki bila kipigo baada ya mechi saba
14h ago
READ MORE β†’
Kamwe awakalia kooni Simba, ashusha tuhuma nzito za sindano
Kamwe awakalia kooni Simba, ashusha tuhuma nzito za sindano
14h ago
READ MORE β†’
Mashujaa hatutegemei kuaminiwa na wengine, tunajiamini wenyewe - Aman Josiah
Mashujaa hatutegemei kuaminiwa na wengine, tunajiamini wenyewe - Aman Josiah
15h ago
READ MORE β†’
Steve Barker aitaka Mashujaa, asema Simba imejipanga kuwania ushindi
Steve Barker aitaka Mashujaa, asema Simba imejipanga kuwania ushindi
15h ago
READ MORE β†’
Ushindi dhidi ya Yanga umetupa jeuri ya kushinda mechi yeyote: Steve Barker
Ushindi dhidi ya Yanga umetupa jeuri ya kushinda mechi yeyote: Steve Barker
16h ago
READ MORE β†’
Aucho atundika daruga timu ya Taifa Uganda baada ya miaka 13
Aucho atundika daruga timu ya Taifa Uganda baada ya miaka 13
16h ago
READ MORE β†’
Barcelona yaongoza kwa utatu wa ushambuliaji wenye takwimu bora Ulaya
Barcelona yaongoza kwa utatu wa ushambuliaji wenye takwimu bora Ulaya
17h ago
READ MORE β†’
Ahmed Ally amchokoza Haji Manara, aomba ridhaa ya kwenda tena Jangwani kuchimba dawa
Ahmed Ally amchokoza Haji Manara, aomba ridhaa ya kwenda tena Jangwani kuchimba dawa
19h ago
READ MORE β†’
Ahmed Ally na Haji Manara wamtetea Mngqithi baada ya kipigo cha dabi
Ahmed Ally na Haji Manara wamtetea Mngqithi baada ya kipigo cha dabi
19h ago
READ MORE β†’