Ligi Kuu y NBC iko kwenye hatua za lala salama ikiwa tayari imeingia kwenye mzunguuko wa 27. Baada ya vibonde KMC kukubali kipigo cha mabao 3-1 dhidi ya Coastal Union jana, mechi nyingine mbili zitapigwa leo.
Namungo Fc watakuwa wenyeji wa TRA United katika mchezo utakaopigwa saa 10 jioni uwanja wa Majaliwa.
Ni vita ya timu mbili zenye malengo tofauti. Namungo Fc wanahitaji ushindi ili kujiondoa katika eneo la hatari kwenye msimamo wa ligi wakati TRA United wanatafuta tiketi ya kushiriki michuano ya CAF msimu ujao.
Azam Fc watachuana na Mashujaa Fc katika mchezo mwingine ambao utapigwa saa 1 usiku.
Mashujaa Fc wametoka kupoteza mchezo uliopita nyumbani dhidi ya Yanga wakifungwa mabao 2-0 wakati Azam Fc walipata ushindi wa mabao 2-0 ugenini dhidi ya Fountain Gate.
Azam Fc kimahesabu bado wako kwenye mbio za ubingwa wakati Mashujaa Fc wanahitaji alama tatu ili kujiweka kwenye eneo salama zaidi katika msimamo.




