Kombe la Dunia la FIFA 2026 linaanza rasmi leo Alhamisi usiku saa 10:00 EAT, ambapo wenyeji na washirika wa uenyeji Mexico watawakaribisha Afrika Kusini katika Uwanja wa kihistoria wa Estadio Azteca, Mexico City, katika mchezo wa Kundi A.
Huu ni mchezo wa ufunguzi wa mashindano mapya yaliyopanuliwa hadi timu 48 na jumla ya michezo 104, hatua inayofanya toleo hili kuwa kubwa zaidi katika historia ya Kombe la Dunia.
Zaidi ya ushindani wa kawaida, mchezo huu una mzigo wa kihisia na historia, ukiwa kurudia kwa mechi ya ufunguzi ya 2010, ambapo Siphiwe Tshabalala aliandika historia kwa bao la mapema kabla Rafael Marquez kusawazisha katika sare ya 1–1 Johannesburg.
Mexico: Historia, presha na matumaini ya kizazi kipya
Mexico wanaingia kwenye mashindano haya wakiwa na hadhi ya kipekee, nchi ya kwanza duniani kuandaa Kombe la Dunia mara tatu (1970, 1986, 2026).
Chini ya kocha Javier Aguirre, anayerejea kwa mara ya tatu, Mexico wanakabiliwa na presha kubwa ya kufanya vizuri nyumbani baada ya kushindwa kuvuka hatua ya makundi Qatar 2022.
Hali ya form kabla ya mashindano
Sare dhidi ya Portugal na Belgium
Ushindi mfululizo wa mechi tatu
Ushindi mkubwa wa 5–1 dhidi ya Serbia
Rekodi nzuri ya kutopoteza mechi 7 za ufunguzi wa Kombe la Dunia (tangu 1994)
Mexico pia wanaingia wakiwa nafasi ya 14 duniani, na wanatarajiwa kumaliza kundi wakiwa juu pamoja na South Korea na Czech Republic.
Wachezaji muhimu wa Mexico
Raúl Jiménez
Mshambuliaji mkongwe na mhimili wa mashambulizi
Goli moja litamfanya afikie 46, akimfikia Jared Borgetti
Silaha ya umaliziaji na uzoefu
Julián Quiñones
Striker mwenye msimu bora Saudi Arabia (33 goals)
Movement kali ndani ya box
Tishio kubwa kwenye nafasi finyu
Edson Álvarez
Nahodha na kiungo wa ulinzi
Atacheza mechi yake ya 99
Kiongozi wa tactical balance
Guillermo Ochoa / Raúl Rangel
Ochoa anaweza kucheza Kombe lake la 6 (rekodi ya kihistoria)
Rangel yupo kwenye ushindani wa namba moja
Uamuzi wake ni muhimu kwa utulivu wa nyuma
Afrika Kusini: Underdogs waliorejea baada ya miaka 16
Afrika Kusini wanarejea Kombe la Dunia kwa mara ya kwanza tangu 2010, baada ya kukosa 2014, 2018 na 2022.
Safari yao ya kufuzu ilikuwa ngumu:
Ushindi wa 3–0 dhidi ya Rwanda siku ya mwisho
Msaada wa matokeo ya Nigeria dhidi ya Benin
Licha ya kupokonywa pointi 3 kwa kosa la mchezaji asiye halali
Chini ya kocha Hugo Broos (tangu 2021), Bafana Bafana wanategemea nidhamu na counter attack.
Rank yao ya FIFA: 60 duniani.
Wachezaji muhimu wa Afrika Kusini
Lyle Foster
Striker wa Burnley (EPL)
Nguvu + kasi + pressing
Tishio kubwa kwenye counter attack
Oswin Appollis
Winga wa Orlando Pirates
Mchango mkubwa kwenye qualifiers (2 goals, 4 assists)
Hatari kwenye 1v1
Teboho Mokoena
Kiungo wa Mamelodi Sundowns
Shots kali na control ya tempo
Engine ya timu
Ronwen Williams
Nahodha na kipa mkuu
Ana uzoefu wa penalti saves
Mchezaji muhimu chini ya presha ya Azteca
Mfumo wa mchezo: Possession vs Counter Attack
Mexico
Possession football
Pressing ya juu
Mashambulizi ya pembeni
Kutegemea umati wa Azteca (83,000)
Afrika Kusini
Low block
Counter attack ya haraka
Set pieces
Nidhamu ya tactical
Vipengele vitakavyoamua mchezo
Jiménez vs Mbokazi/Okon (ulinzi wa kati)
Appollis vs fullbacks wa Mexico (pace battle)
Mokoena vs Álvarez (control ya midfield)
Uamuzi wa kipa wa Mexico (Ochoa vs Rangel)
Presha ya mashabiki wa Azteca
Takwimu muhimu
Mexico: clean sheets 6 katika mechi 8 za mwisho
Afrika Kusini: wamefunga katika mechi 9 kati ya 11
BTTS (both teams to score): 5 kati ya 6 mechi za mwisho kwa pande zote
Utabiri wa mchezo
Huu ni mchezo mgumu kuliko unavyoonekana kwenye karatasi:
Mexico wana faida ya nyumbani + uzoefu wa Kombe la Dunia
Afrika Kusini ni hatari kwenye counter attack
Azteca itaongeza presha kubwa kwa wageni
Utabiri wa mchezo
Mexico watatawala umiliki wa mpira na wana nafasi kubwa ya kushinda
Afrika Kusini watapata nafasi zao kupitia mashambulizi ya kujibu.
Mchezo unaweza kubadilika kama Bafana wakifunga kwanza



