Simba, Chamou mwisho umefika

Joel JJ By Joel JJ β€’ 6th June 2026


Simba, Chamou mwisho umefika

Klabu ya Simba SC haina mpango wa kuendelea na beki raia wa Ivory Coast Carabou Chamou, akiwa sio sehemu ya mipango ya timu hiyo kwa msimu ujao.

Inaelezwa kuwa viongozi wa Simba tayari wamemuarifu mchezaji huyo kuhusu msimamo wa klabu, hatua inayompa nafasi ya kuanza kutafuta changamoto mpya kabla ya kufunguliwa kwa dirisha kubwa la usajili mwezi ujao.

Chamoua kwa sasa anaitumikia TRA United FC kwa mkopo, ambapo ameendelea kupata muda wa kucheza baada ya kushindwa kupata nafasi ya kudumu ndani ya kikosi cha Wekundu wa Msimbazi msimu huu.

Mkataba wa beki huyo na Simba unatarajiwa kumalizika mwishoni mwa mwezi huu. Wakati huo huo, TRA United inatajwa kuridhishwa na mchango wake na inaonyesha nia ya kuendelea kuwa naye kwa muda mrefu zaidi.

Chamoua alikuwa miongoni mwa wachezaji waliosajiliwa katika msimu wa 2024/25 wakati Simba ilipoanza mchakato wa kujenga kikosi kipya chini ya kocha Fadlu Davids. Hata hivyo, ushindani mkubwa wa nafasi ndani ya kikosi ulimfanya ashindwe kupata nafasi ya mara kwa mara.

Pamoja na Chamoua, kiungo Mzamiru Yassin pia anakabiliwa na hatma inayofanana. Mchezaji huyo naye anatarajiwa kumaliza mkataba wake mwishoni mwa mwezi huu, huku taarifa zikieleza kuwa hana nafasi katika mipango ya Simba ya msimu ujao.


  

XTRA 90 INSIDER

Get the latest tactics & rumors delivered to your inbox.