Tetesi za usajili Ulaya Jumatano, Julai 16 2025

Joel JJ By Joel JJ
β€’
16 Jul 2025
Tetesi za usajili Ulaya Jumatano, Julai 16 2025

Liverpool inatarajiwa kumenyana na Newcastle United katika kinyang'anyiro cha mshambuliaji wa Eintracht Frankfurt Mfaransa Hugo Ekitike, 23, baada ya kufahamishwa kuwa mshambuliaji wa Uswidi Alexander Isak, 25, hatahama klabu yake katika dirisha hili la usajili. (Sky Sports)

The Magpies inahisi kuvujishwa kwa ofa ya Liverpool ya pauni milioni 120 kulilenga kumtatiza Isak. (Telegraph - usajili unahitajika)

Pamoja na Ekitike, Liverpool pia inawafukuzia washambuliaji wengine wanne endapo itamkosa Isak - wachezaji hao ni pamoja na Ollie Watkins wa Aston Villa, 29, Victor Osimhen wa Napoli, 26, Yoane Wissa wa Brentford, 28, na Rodrygo wa Real Madrid, 24. (Mail+ - usajili unahitajika)

Napoli imefahamisha Liverpool kwamba dili la kumsajili mshambuliaji wa Uruguay Darwin Nunez, 26, linaweza kusitishwa. (Fabrizio Romano)

Winga wa Colombia Luis Diaz, 28, ameweka wazi kuwa anataka kuondoka kwa Reds baada ya klabu hiyo kukataa dau la pauni milioni 58.6 kutoka kwa Bayern Munich. (Athletic - michango inahitajika)

Leeds United imefikia makubaliano ya awali ya kumsajili kiungo wa Newcastle Muingereza Sean Longstaff, 27. (Athletic- Usajili unahitajika)

Tottenham inachuana na Inter Milan kumsajili beki wa Ubelgiji Koni de Winter, 23. (i paper)

Bournemouth imewasilisha dau la pauni milioni 59 kumsajili beki wa Ukraine Illia Zabaryni, 22, ambaye anasakwa na Paris St-Germain. (Independent)

Chelsea iko tayari kuanza mchujo wa msimu wa kiangazi huku mshambuliaji wa Ureno Joao Felix, 25, akiwa katika mazungumzo ya kurejea Benfica na Mfaransa Christopher Nkunku, 27, pia anatarajiwa kuondoka. (Standard)

Manchester United imewasilisha rasmi ombi la kumsajili kiungo wa Juventus na Mbrazil Douglas Luiz msimu huu kiangazi, huku Everton pia ikimnyatia mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27. (Football Insider)

Beki wa Liverpool na Ufaransa Ibrahima Konate, 26, amekataa ofa ya kujiunga na klabu ya Ligi Kuu ya Saudi Pro. (Mirror)

The Reds imeweka bei ya pauni milioni 43.5 kwa Konate kwa vilabu vyovyote vinavyotaka kusajili mchezaji huyo msimu huu wa kiangazi. (AS - kwa Kihispania)

Mshambuliaji wa klabu ya Sassuolo na Italia, Andrea Pinamonti ananyatiwa na klavu ya Ligi ya Premia West Ham, huku wapinzani wa London Brentford pia wakiulizia kuhusu mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26. (Standard)

Leeds United ina nia ya kumsajili mshambuliaji wa Uhispania Gonzalo Garcia, 21, kwa mkopo kutoka Real Madrid. (TBR Football)

BBC

ADVERTISE HERE

More Stories

Natumaini Caf itaidhinisha uhuru stadium kwa mechi za makundi : Wallace Karia
Natumaini Caf itaidhinisha uhuru stadium kwa mechi za makundi : Wallace Karia
36m ago
READ MORE β†’
Azam FC yaibuka na ushindi ugenini dhidi ya JKT Tanzania
Azam FC yaibuka na ushindi ugenini dhidi ya JKT Tanzania
58m ago
READ MORE β†’
Brighton yaizamisha Manchester City Etihad, mbio za ubingwa zazidi kupamba moto
Brighton yaizamisha Manchester City Etihad, mbio za ubingwa zazidi kupamba moto
1h ago
READ MORE β†’
Orlando Pirates yawasha moto kwenye dabi ya Soweto, Simba yapata onyo
Orlando Pirates yawasha moto kwenye dabi ya Soweto, Simba yapata onyo
2h ago
READ MORE β†’
Manchester United yaendeleza mwenendo mbaya baada ya kichapo kutoka Chelsea
Manchester United yaendeleza mwenendo mbaya baada ya kichapo kutoka Chelsea
3h ago
READ MORE β†’
Gamondi aita kikosi cha kuikabili Nigeria kufuzu Afcon 2027
Gamondi aita kikosi cha kuikabili Nigeria kufuzu Afcon 2027
5h ago
READ MORE β†’
Ligi kuu bara kuendelea leo, Mkwakwani na Isamuhyo kuwaka moto
Ligi kuu bara kuendelea leo, Mkwakwani na Isamuhyo kuwaka moto
8h ago
READ MORE β†’
Dladla awataka mashabiki wa Yanga kujitokeza kwa wingi kuiunga mkono timu yao
Dladla awataka mashabiki wa Yanga kujitokeza kwa wingi kuiunga mkono timu yao
9h ago
READ MORE β†’
Tunatarajia mchezo mgumu, lakini lengo letu ni ubingwa: Dladla kocha yanga
Tunatarajia mchezo mgumu, lakini lengo letu ni ubingwa: Dladla kocha yanga
9h ago
READ MORE β†’
Wikiendi ya moto: Mechi kubwa sita kutawala viwanja vya soka
Wikiendi ya moto: Mechi kubwa sita kutawala viwanja vya soka
10h ago
READ MORE β†’