Tetesi za usajili Ulaya, Jumatano, May 21 2025

Joel JJ By Joel JJ
β€’
21 May 2025
Tetesi za usajili Ulaya, Jumatano, May 21 2025

Newcastle United ni miongoni mwa vilabu vinavyotarajiwa kufanya mazungumzo na mshambuliaji wa Ipswich Town mwenye umri wa miaka 22 Liam Delap wiki hii. (Talk sport)

Manchester United wanaongoza katika kinyang'anyiro cha kumsajili Delap lakini kushindwa katika fainali ya Ligi ya Europa na kutoweza kumpatia soka la Ulaya msimu ujao kutaipa Chelsea faida. (ESPN)

Manchester City itamenyana na Liverpool kuwania saini ya Mchezaji wa Bournemouth mwenye umri wa miaka 21 na beki wa kushoto wa Hungary Milos Kerkez. (i paper- usajili unahitajika)

Brighton imekubali kumsajili beki wa Ufaransa Olivier Boscagli, 27, kwa uhamisho wa bure kutoka PSV Eindhoven. (Sky Sports)

Liverpool imepokea maombi kutoka kwa Ligi ya Sudia kumhusumshambuliaji wa Uruguay Darwin Nunez, mshambuliaji wa Ureno Diogo Jota na winga wa Colombia Luis Diaz. (Sky Germany)

Manchester United iko tayari kulipa ada ya kuachiliwa kwa mshambuliaji wa Brazil Matheus Cunha (25) kwa awamu. (Fabrizio Romano)

Manchester United pia inapania kumshawishi mshambuliaji wa klabu ya Sporting na timu ya taifa ya Uswidi Viktor Gyokeres, 26, kujiunga nao msimu huu wa kiangazi. (L'Equipe - kwa kifaransa)

Aston Villa haina nia ya kumzuia kipa wa Argentina Emiliano Martinez, 32, ikiwa anataka kuondoka Villa Park. (Givemesport)

Chelsea iko tayari kwa mazungumzo na klabu ya Ajax kuhusu uhamisho wa mlinzi wa Uholanzi Jorrel Hato, 19, ambaye pia ananyatiwa na Liverpool na Arsenal. (Caughtoffside)

Barcelona imefikia mkataba mpya na mshambuliaji wa Brazil Raphinha (28) ambao utamuwezesha kusalia katika klabu hiyo hadi mwezi Juni 2028. (Fabrizio Romano)

Mkufunzi wa Nottingham Forest Nuno Espirito Santo huenda akaondoka mwishoni mwa nsimu huu kufuatia mvutano wa ndani ya klabu hiyo. (Footmercato - kwa kifaransa)

Leicester City wanatarajiwa kumtimua kocha wao Ruud van Nistelrooy huku mpango wa kumsajili meneja wa zamani wa Southampton Russell Martin ukipiga hatua. (Football Insider)

BBC

ADVERTISE HERE

More Stories

Natumaini Caf itaidhinisha uhuru stadium kwa mechi za makundi : Wallace Karia
Natumaini Caf itaidhinisha uhuru stadium kwa mechi za makundi : Wallace Karia
12m ago
READ MORE β†’
Azam FC yaibuka na ushindi ugenini dhidi ya JKT Tanzania
Azam FC yaibuka na ushindi ugenini dhidi ya JKT Tanzania
34m ago
READ MORE β†’
Brighton yaizamisha Manchester City Etihad, mbio za ubingwa zazidi kupamba moto
Brighton yaizamisha Manchester City Etihad, mbio za ubingwa zazidi kupamba moto
1h ago
READ MORE β†’
Orlando Pirates yawasha moto kwenye dabi ya Soweto, Simba yapata onyo
Orlando Pirates yawasha moto kwenye dabi ya Soweto, Simba yapata onyo
2h ago
READ MORE β†’
Manchester United yaendeleza mwenendo mbaya baada ya kichapo kutoka Chelsea
Manchester United yaendeleza mwenendo mbaya baada ya kichapo kutoka Chelsea
2h ago
READ MORE β†’
Gamondi aita kikosi cha kuikabili Nigeria kufuzu Afcon 2027
Gamondi aita kikosi cha kuikabili Nigeria kufuzu Afcon 2027
5h ago
READ MORE β†’
Ligi kuu bara kuendelea leo, Mkwakwani na Isamuhyo kuwaka moto
Ligi kuu bara kuendelea leo, Mkwakwani na Isamuhyo kuwaka moto
7h ago
READ MORE β†’
Dladla awataka mashabiki wa Yanga kujitokeza kwa wingi kuiunga mkono timu yao
Dladla awataka mashabiki wa Yanga kujitokeza kwa wingi kuiunga mkono timu yao
8h ago
READ MORE β†’
Tunatarajia mchezo mgumu, lakini lengo letu ni ubingwa: Dladla kocha yanga
Tunatarajia mchezo mgumu, lakini lengo letu ni ubingwa: Dladla kocha yanga
8h ago
READ MORE β†’
Wikiendi ya moto: Mechi kubwa sita kutawala viwanja vya soka
Wikiendi ya moto: Mechi kubwa sita kutawala viwanja vya soka
10h ago
READ MORE β†’