Tetesi za soka Ulaya, Alhamisi Januari 30 2025

Joel JJ By Joel JJ
β€’
30 Jan 2025
Tetesi za soka Ulaya, Alhamisi Januari 30 2025

Arsenal wanatarajiwa kufanya jaribio la pili lililo bora zaidi kumsajili mshambuliaji wa Aston Villa na England Ollie Watkins, 29, ambaye alikua shabiki wa Gunners. (Mail)

Manchester United wako kwenye mazungumzo ya muda na Barcelona kuhusu uhamisho wa mkopo wa mshambuliaji wa Uingereza Marcus Rashford, 27, lakini kuna wasiwasi wa iwapo klabu hiyo ya Uhispania itaweza kukamilisha dili kabla ya tarehe ya mwisho ya Jumatatu. (Telegraph - Subscription Required)

Vilabu vya Ujerumani Bayern Munich na Borussia Dortmund vimeungana na Tottenham katika mbio za kumsajili winga wa Southampton Mwingereza mwenye umri wa miaka 18 Tyler Dibling. (Sun)

Mshambulizi wa Colombia Jhon Duran, 21, anatarajiwa kufanyiwa uchunguzi wa kimatibabu mjini London siku ya Alhamisi kabla ya pendekezo la euro 77m (£64m) pamoja na kuondoka Villa kuhamia Al Nassr. (Athletic - Subscription Required)

Arsenal wako tayari kuipatia Bayern Munich ofa ya mshambuliaji wa Ufaransa chini ya umri wa miaka 21 Mathys Tel, 19, kabla ya kufungwa kwa dirisha la usajili la Januari. (Football Transfers)

The Gunners na Chelsea wote wanachunguza uhamisho wa Tel, huku Manchester United pia wakifuatilia hali ya mchezaji huyo. (Independent)

Tottenham pia wana nia ya kumsaini Tel kwa mkopo mwezi huu. (Mail)

Napoli wamekataa dau la euro 65m (£54.5m) kutoka kwa Galatasaray kufanya uhamisho wa mkopo wa mshambuliaji wa Nigeria Victor Osimhen, 26, kuwa wa kudumu. (Corriere dello Sport - In Italy)

Newcastle United wanatazamiwa kuzishinda klabu kadhaa za Premier League kumsajili winga wa kimataifa wa vijana wa Jamhuri ya Ireland Kyle Fitzgerald kutoka Galway United, 18. (Football Insider)

Napoli wamemuarifu winga wa Argentina mwenye umri wa miaka 20 Alejandro Garnacho kwamba watakuwa tayari kujaribu kumsajili tena ikiwa Manchester United itapunguza mahitaji yao. (Fabrizio Romano)

Steven Gerrard ameripotiwa kuomba kuondoka kwenye klabu ya Saudia Pro League Al Ettifaq baada ya miezi 18, kulingana na ripoti kutoka Saudi Arabia. (Mirror)

Torino ndio wanaopewa nafasi kubwa ya kumsajili kiungo wa kati wa Chelsea na Muitaliano Cesare Casadei, 22, huku Lazio sasa ikiwa nje ya mbio hizo. (Gianlucadimarzio - In Italy)

BBC

ADVERTISE HERE

More Stories

Manchester United yaendeleza mwenendo mbaya baada ya kichapo kutoka Chelsea
Manchester United yaendeleza mwenendo mbaya baada ya kichapo kutoka Chelsea
46m ago
READ MORE β†’
Gamondi aita kikosi cha kuikabili Nigeria kufuzu Afcon 2027
Gamondi aita kikosi cha kuikabili Nigeria kufuzu Afcon 2027
3h ago
READ MORE β†’
Ligi kuu bara kuendelea leo, Mkwakwani na Isamuhyo kuwaka moto
Ligi kuu bara kuendelea leo, Mkwakwani na Isamuhyo kuwaka moto
5h ago
READ MORE β†’
Dladla awataka mashabiki wa Yanga kujitokeza kwa wingi kuiunga mkono timu yao
Dladla awataka mashabiki wa Yanga kujitokeza kwa wingi kuiunga mkono timu yao
6h ago
READ MORE β†’
Tunatarajia mchezo mgumu, lakini lengo letu ni ubingwa: Dladla kocha yanga
Tunatarajia mchezo mgumu, lakini lengo letu ni ubingwa: Dladla kocha yanga
6h ago
READ MORE β†’
Wikiendi ya moto: Mechi kubwa sita kutawala viwanja vya soka
Wikiendi ya moto: Mechi kubwa sita kutawala viwanja vya soka
8h ago
READ MORE β†’
Jeraha la Kariakoo derby lamuondoa Duke Abuya Harambee stars
Jeraha la Kariakoo derby lamuondoa Duke Abuya Harambee stars
9h ago
READ MORE β†’
CAF yamchagua Arajiga miongoni mwa waamuzi 35 kupata mafunzo maalum Cairo
CAF yamchagua Arajiga miongoni mwa waamuzi 35 kupata mafunzo maalum Cairo
9h ago
READ MORE β†’
Hoja tano zinazoweza kuboresha tuzo ya Ballon d’Or
Hoja tano zinazoweza kuboresha tuzo ya Ballon d’Or
21h ago
READ MORE β†’
Samatta katika mtihani mzito: Le Havre ikiikaribisha PSG leo
Samatta katika mtihani mzito: Le Havre ikiikaribisha PSG leo
1d ago
READ MORE β†’