Tetesi za usajili Ulaya Jumatano, Disemba 11 2024

Joel JJ By Joel JJ
β€’
11 Dec 2024
Tetesi za usajili Ulaya Jumatano, Disemba 11 2024

Manchester United inataka kumuuza mshambuliaji wa Uingereza Marcus Rashford, 27, katika dirisha la uhamisho la Januari. (Sky Sport Germany)

United walikuwa tayari kumuuza Rashford aliyehitimu katika akademia yao msimu uliopita na sasa wanapokea ofa mpya. (Telegraph – Subscription Required)

The Red Devils pia wanaweza kumuuza Lisandro Martinez ikiwa Real Madrid itaongeza nia yao ya kumnunua beki huyo wa Argentina, 26. (Talksport)

Arsenal wanafikiria kumnunua mshambuliaji wa Serbia mwenye umri wa miaka 24 Dusan Vlahovic kutoka Juventus Januari. (TeamTalk)

Beki wa kati wa Uholanzi Virgil van Dijk, 33, yuko tayari kusaini mkataba mpya na Liverpool licha ya kukataa ofa ya awali. (Football Insider)

&Newcastle United inamfuatilia winga wa PSV Eindhoven wa Ubelgiji Johan Bakayoko, 21, kabla ya dirisha la uhamisho la Januari. (Telegraph – Subscription Required)

Barcelona wanaweza tu kumsajili Dani Olmo msimu wa ujao kucheza La Liga hadi Disemba 31, lakini fowadi huyo wa Uhispania, 26, atakuwa mchezaji huru ikiwa Barca hawatamsajili tena Januari. (Mundo Deportivo – In Spanish)

Arsenal wana hamu ya kumsajili Dan Ashworth kama mkurugenzi wao mpya wa michezo baada ya kuondoka Manchester United. (ESPN) Mazungumzo ya Liverpool kuhusu mkataba mpya na mshambuliaji wa Misri Mohamed Salah, 32, yanaendelea huku pande hizo mbili zikikaribia kuafikiana kuhusu muundo mpya wa malipo. (Sky Sports)

AC Milan wako tayari kumruhusu nahodha Theo Hernandez kuondoka katika klabu hiyo lakini watadai ada ya takriban £41m kwa beki huyo wa kushoto wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 27. (Calciomercato - Itali)

Chelsea haitafikiria kumruhusu mlinzi wa kati Tosin Adarabioyo mwenye umri wa miaka 27 kuondoka kwa mkopo mwezi Januari huku kukiwa na taarifa za yeye kutaka kuelekea West Ham. (Football Insider)

Kiungo wa kati wa Denmark Christian Eriksen, 32, anatarajiwa kuondoka Manchester United mwishoni mwa msimu huu. (Fabrizio Romano) Aston Villa wanafikiria kumwita Louie Barry, 21, kutoka kwa mkopo katika League One Stockport County ili kumpeleka mshambuliaji huyo wa Uingereza mwenye mabao 14 kwa klabu iliyo katika kiwango cha juu zaidi. (TeamTalk)

BBC

ADVERTISE HERE

More Stories

De Klassiker hakuna mshindi, Bayern 2-2 Dortmund
De Klassiker hakuna mshindi, Bayern 2-2 Dortmund
1h ago
READ MORE β†’
Natumaini Caf itaidhinisha uhuru stadium kwa mechi za makundi : Wallace Karia
Natumaini Caf itaidhinisha uhuru stadium kwa mechi za makundi : Wallace Karia
3h ago
READ MORE β†’
Azam FC yaibuka na ushindi ugenini dhidi ya JKT Tanzania
Azam FC yaibuka na ushindi ugenini dhidi ya JKT Tanzania
3h ago
READ MORE β†’
Brighton yaizamisha Manchester City Etihad, mbio za ubingwa zazidi kupamba moto
Brighton yaizamisha Manchester City Etihad, mbio za ubingwa zazidi kupamba moto
4h ago
READ MORE β†’
Orlando Pirates yawasha moto kwenye dabi ya Soweto, Simba yapata onyo
Orlando Pirates yawasha moto kwenye dabi ya Soweto, Simba yapata onyo
4h ago
READ MORE β†’
Manchester United yaendeleza mwenendo mbaya baada ya kichapo kutoka Chelsea
Manchester United yaendeleza mwenendo mbaya baada ya kichapo kutoka Chelsea
5h ago
READ MORE β†’
Gamondi aita kikosi cha kuikabili Nigeria kufuzu Afcon 2027
Gamondi aita kikosi cha kuikabili Nigeria kufuzu Afcon 2027
8h ago
READ MORE β†’
Ligi kuu bara kuendelea leo, Mkwakwani na Isamuhyo kuwaka moto
Ligi kuu bara kuendelea leo, Mkwakwani na Isamuhyo kuwaka moto
10h ago
READ MORE β†’
Dladla awataka mashabiki wa Yanga kujitokeza kwa wingi kuiunga mkono timu yao
Dladla awataka mashabiki wa Yanga kujitokeza kwa wingi kuiunga mkono timu yao
11h ago
READ MORE β†’
Tunatarajia mchezo mgumu, lakini lengo letu ni ubingwa: Dladla kocha yanga
Tunatarajia mchezo mgumu, lakini lengo letu ni ubingwa: Dladla kocha yanga
11h ago
READ MORE β†’