Kocha wa zamani wa klabu za Mbeya City na Yanga, Juma Mwambusi amejiunga na Coastal Union
Taarifa kutoka ndani ya uongozi wa Coastal Union, zimethibitisha kuwa Mwambusi amepewa mkataba wa mwaka mmoja kuwanoa wagosi hao wa Kaya na tayari ametua jijini Arusha kuanza majukumu yake
Coastal Union inacheza mechi zake za nyumbani uwanja wa Sheikh Amri Abeid, wakati uwanja wa Mkwakwani ukifanyiwa ukarabati mkubwa
Timu yake ya mwisho kuifundisha kabla ya kutangaza kupumzika masuala ya ukocha kwa muda ilikuwa Ihefu Fc (sasa Singida BS)
ADVERTISE HERE