Tetesi za usajili Ulaya, Jumatano Septemba 04 2024

Joel JJ By Joel JJ
β€’
4 Sep 2024
Tetesi za usajili Ulaya, Jumatano Septemba 04 2024

Galatasaray wapo kwenye mazungumzo na Manchester United kuhusu uhamisho wa mkopo wa mwaka mmoja kwa kiungo wao wa kati wa Brazil Casemiro, 32. (Ali Naci Kucuk – In Turkish)

Liverpool wanapanga kufanya mazungumzo ya kandarasi na mshambuliaji wa Misri Mohamed Salah, 32, baada ya kusema huu ulikuwa "msimu wake wa mwisho" katika klabu hiyo kufuatia ushindi wao dhidi ya Manchester United. (Football Insider)

Meneja wa Pumas UNAM Gustavo Lema anasema Liverpool ilijaribu kumsajili winga wao wa Mexico Cesar Huerta, 23. (TUDN – In Spanish)

Chelsea wako tayari kumtuma beki wa kushoto wa Uingereza Ben Chilwell, 27, kwa mkopo Uturuki, ingawa bado hawajapokea ofa yoyote. (Telegraph – Subscription Required)

Mazungumzo yanaendelea kati ya Chelsea na AEK Athens kuhusu uhamisho wa mshambuliaji wa Ivory Coast David Datro Fofana, 21. (Mail) Tottenham wamefanya mazungumzo ya kumnunua kiungo wa kati wa Marekani Johnny Cardoso, 22, kwa £21m kutoka Real Betis. (Telegraph – Subscription Required)

Kiungo wa kati wa zamani wa Liverpool Naby Keita, 29, yuko kwenye mazungumzo na Istanbul Basaksehir kuhusu uwezekano wa kuhama kutoka Werder Bremen baada ya mchezaji huyo wa kimataifa wa Guinea kutokubaliana na masharti ya kuhamia Sunderland. (Guardian)

Winga wa zamani wa Manchester United Anthony Martial, 28, amepewa mkataba na AEK Athens ambao utamfanya kuwa mchezaji anayelipwa pesa nyingi zaidi klabuni hapo. Mfaransa huyo alikua mchezaji huru wakati kandarasi yake United ilipoisha mwezi Juni. (Sport24 via Sun)

Manchester United inamfuatilia kwa karibu beki wa kushoto wa Juventus mwenye umri wa miaka 23 kutoka Colombia Juan Cabal. (Tutto Juve – In Italy)

Real Betis walitoa ofa kwa kiungo wa kati wa Manchester United na Denmark Christian Eriksen, 32, siku ya mwisho ya dirisha la uhamisho (Fabrizio Romano)

BBC

 

ADVERTISE HERE

More Stories

Gamondi aita kikosi cha kuikabili Nigeria kufuzu Afcon 2027
Gamondi aita kikosi cha kuikabili Nigeria kufuzu Afcon 2027
50m ago
READ MORE β†’
Ligi kuu bara kuendelea leo, Mkwakwani na Isamuhyo kuwaka moto
Ligi kuu bara kuendelea leo, Mkwakwani na Isamuhyo kuwaka moto
2h ago
READ MORE β†’
Dladla awataka mashabiki wa Yanga kujitokeza kwa wingi kuiunga mkono timu yao
Dladla awataka mashabiki wa Yanga kujitokeza kwa wingi kuiunga mkono timu yao
3h ago
READ MORE β†’
Tunatarajia mchezo mgumu, lakini lengo letu ni ubingwa: Dladla kocha yanga
Tunatarajia mchezo mgumu, lakini lengo letu ni ubingwa: Dladla kocha yanga
4h ago
READ MORE β†’
Wikiendi ya moto: Mechi kubwa sita kutawala viwanja vya soka
Wikiendi ya moto: Mechi kubwa sita kutawala viwanja vya soka
5h ago
READ MORE β†’
Jeraha la Kariakoo derby lamuondoa Duke Abuya Harambee stars
Jeraha la Kariakoo derby lamuondoa Duke Abuya Harambee stars
6h ago
READ MORE β†’
CAF yamchagua Arajiga miongoni mwa waamuzi 35 kupata mafunzo maalum Cairo
CAF yamchagua Arajiga miongoni mwa waamuzi 35 kupata mafunzo maalum Cairo
6h ago
READ MORE β†’
Hoja tano zinazoweza kuboresha tuzo ya Ballon d’Or
Hoja tano zinazoweza kuboresha tuzo ya Ballon d’Or
19h ago
READ MORE β†’
Samatta katika mtihani mzito: Le Havre ikiikaribisha PSG leo
Samatta katika mtihani mzito: Le Havre ikiikaribisha PSG leo
1d ago
READ MORE β†’
Chelsea na Manchester united katika vita ya alama tatu kesho Stamford Bridge
Chelsea na Manchester united katika vita ya alama tatu kesho Stamford Bridge
1d ago
READ MORE β†’