Tetesi za usajili Ulaya, Alhamisi, August 08 2024

Joel JJ By Joel JJ
β€’
8 Aug 2024
Tetesi za usajili Ulaya, Alhamisi, August 08 2024

Manchester United wanaweza kumjaribu kiungo wa kati wa Burnley na Norway Sander Berge, 26, kwenda Old Trafford kwa kumpa kandarasi ya pauni 100,000 kwa wiki. (Sun)

West Ham wanavutiwa na beki wa kulia wa Uingereza Kieran Trippier, huku mustakabali wa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 33 huko Newcastle bado haujaamuliwa. (Telegraph – Subscription Required)

Chelsea wamekubali mkataba wa pauni milioni 35 na Atletico Madrid kumsajili mshambuliaji wa Uhispania Samu Omorodion, na mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 20 anatazamiwa kufanyiwa uchunguzi wa kimatibabu. (Fabrizio Romano)

Kiungo wa kati wa Uhispania Martin Zubimendi anatarajiwa na Real Sociedad kukubali kuhamia Liverpool, ingawa vilabu bado vinahitaji kuafikiana dili la mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25. (Athletic – Subscription Required)

Mshambulizi wa Chelsea na Albania Armando Broja atafanya mazungumzo na meneja Enzo Maresca kufahamu mustakabali wake. Everton na Wolves ni miongoni mwa wanaomtaka mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22. (Mail)

West Ham wanavutiwa na mlinzi wa Chelsea Muingereza Trevoh Chalobah, 26, na beki wa kati wa Ujerumani Mats Hummels, 35, ambaye ni mchezaji huru baada ya kuondoka Borussia Dortmund. (Sky Sports)

Crystal Palace pia inamtazama mlinzi wa Chelsea Chalobah, na mlinzi wa Wolfsburg ya Ufaransa Maxence Lacroix, 24, kama chaguo la beki wa kati. (Telegraph – Subscription Required)

Chelsea wamewasiliana na Rangers kuhusu uwezekano wa kumnunua kiungo wa kati wa akademi mwenye umri wa miaka 19 Leo Castledine. Aberdeen pia wanavutiwa na Mwingereza huyo. (FootballScotland)

Liverpool bado wanavutiwa na mshambuliaji wa Ujerumani na Hoffenheim Maximilian Beier, lakini mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21 anataka kujiunga na Borussia Dortmund na yuko kwenye mazungumzo na klabu hiyo ya Bundesliga. (Sky Germany)

Southampton wamepokea ofa kutoka Hoffenheim kwa mlinzi wa miaka 22 Armel Bella-Kotchap. The Saints tayari wamekataa ofa ya £8.6m kutoka Stuttgart. (Sky Germany)

Beki wa Aston Villa Lucas Digne amekataa pendekezo la kujiunga na Galatasaray. Mfaransa huyo mwenye umri wa miaka 31 anatarajiwa kubaki na Villa. (Athletic – Subscription Required} Brentford wanakaribia kumsajili kiungo wa kati wa Uswidi Jens Cajuste, 24, kwa mkopo kutoka Napoli. (Sky Sports)

Fiorentina wamekuwa wakiwasiliana kuhusu uwezekano wa kumnunua kipa wa zamani wa Uhispania na Manchester United David de Gea, 33. (Football Italia)

Valencia inaonekana kujiondoa katika mazungumzo kuhusu pendekezo la kiungo wa kati wa Uhispania Javi Guerra kwenda Atletico Madrid, 21. (Athletic – Subscription Required)

Leicester City wamefanya uchunguzi na Ajax kuhusu upatikanaji wa mshambuliaji wa Uholanzi Steven Bergwijn, 26. (Fabrizio Romano)

BBC

ADVERTISE HERE

More Stories

Matola: Namungo ni timu imara, tunataka kutetea rekodi yetu
Matola: Namungo ni timu imara, tunataka kutetea rekodi yetu
3h ago
READ MORE β†’
Tunakwenda kucheza na timu mzito na ngumu: Juma Mgunda
Tunakwenda kucheza na timu mzito na ngumu: Juma Mgunda
3h ago
READ MORE β†’
Jack Grealish aingia matatani Everton baada ya kuripotiwa kula bata siku mbili mfululizo
Jack Grealish aingia matatani Everton baada ya kuripotiwa kula bata siku mbili mfululizo
3h ago
READ MORE β†’
NBC Premier League: Mechi mbili za kibabe kupigwa leo.
NBC Premier League: Mechi mbili za kibabe kupigwa leo.
5h ago
READ MORE β†’
Wikiendi ya mechi kubwa inaendelea: Liverpool vs Arsenal na Napoli vs Juventus
Wikiendi ya mechi kubwa inaendelea: Liverpool vs Arsenal na Napoli vs Juventus
6h ago
READ MORE β†’
De Klassiker hakuna mshindi, Bayern 2-2 Dortmund
De Klassiker hakuna mshindi, Bayern 2-2 Dortmund
18h ago
READ MORE β†’
Natumaini Caf itaidhinisha uhuru stadium kwa mechi za makundi : Wallace Karia
Natumaini Caf itaidhinisha uhuru stadium kwa mechi za makundi : Wallace Karia
20h ago
READ MORE β†’
Azam FC yaibuka na ushindi ugenini dhidi ya JKT Tanzania
Azam FC yaibuka na ushindi ugenini dhidi ya JKT Tanzania
20h ago
READ MORE β†’
Brighton yaizamisha Manchester City Etihad, mbio za ubingwa zazidi kupamba moto
Brighton yaizamisha Manchester City Etihad, mbio za ubingwa zazidi kupamba moto
21h ago
READ MORE β†’
Orlando Pirates yawasha moto kwenye dabi ya Soweto, Simba yapata onyo
Orlando Pirates yawasha moto kwenye dabi ya Soweto, Simba yapata onyo
22h ago
READ MORE β†’