Tetesi za usajili Ulaya, Jumatano, May 29 2024

Joel JJ By Joel JJ
β€’
29 May 2024
Tetesi za usajili Ulaya, Jumatano, May 29 2024

Klabu kadhaa za ligi kuu ya Saudia (Saudi Pro), ikiwemo Al Nassr, Al Ahli na Al Qasidiya, zinawania kumsajili kiungo wa kati wa timu ya taifa ya Brazil Casemiro, 32, kutoka Manchester United msimu huu. (Goal - kwa Kireno)

West Ham wamefikia mkataba wa pauni milioni 15 na Flamengo kumnunua mlinzi wa Brazil Fabricio Bruno, 28. (Guardian)

Mshambuliaji wa Manchester United Muingereza Mason Greenwood anataka kurejea katika klabu ya Getafe ya Uhispania msimu ujao baada ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 hivi majuzi kucheza mechi yake ya mwisho kama mchezaji wa mkopo katika klabu hiyo ya La Liga. (TEAMtalk)

Aston Villa na Crystal Palace wanatazamia kumnunua beki wa Gent Muingereza Archie Brown, 22. (Mirror)

Barcelona huenda wakamrejesha Nou Camp kwa mara ya pili mshambuliaji wa Ureno Joao Felix kutoka Atletico Madrid. (Sport - kwa Kihispania)

Newcastle wanashinikiza kupata jibu kuhusu uwezekano wa kumnunua beki wa Uingereza Tosin Adarabioyo, huku mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 akitarajiwa kuondoka Fulham msimu huu wa joto mkataba wake utakapomalizika. (Talksport)

Liverpool wameweka thamani ya pauni milioni 20 kwa mlinzi wa Uholanzi Sepp van den Berg, 22, ambaye ananyatiwa na klabu za Brentford, Southampton na Wolfsburg baada ya kung'aa alipokuwa Mainz kwa mkopo . (Athletic, usajili unahitajika)

Napoli hawana nia ya kumuuza winga wa Georgia Khvicha Kvaratskhelia, 23, kwa Paris St-Germain, huku Antonio Conte akitarajiwa kuwa kocha wao mkuu mpya. (Corriere dello Sport kwa Kiitaliano)

Mshambuliaji wa Real Madrid wa Brazil Rodrygo, 23, ametilia shaka mustakabali wake katika klabu hiyo, na hivyo kuongeza uwezekano wa kuhamia Liverpool. (Mundo Deportivo - kwa Kihispania, kupitia Dazn)

Southampton wanawania saini ya winga wa Sunderland Muingereza Jack Clarke, 23. (Telegraph - usajili unahitajika)

Inter Milan wanavutiwa na beki Mwingereza Aaron Wan-Bissaka, 26, ambaye Manchester United imeweka thamani yake kuwa euro 12m (Β£10.2m). (Tuttomercatoweb - kwa Kiitaliano)

Arsenal na kocha Mikel Arteta wapo kwenye mazungumzo kuhusu mkataba mpya wa kudumu katika klabu hiyo. (Football Insider)

Nia ya Xavi ya kumuuza mshambuliaji wa Poland Robert Lewandowski mwenye umri wa miaka 35 msimu huu ilikuwa sababu kuu ya Mhispania huyo kufukuzwa kazi Barcelona mwezi huu. (Sport - kwa Kihispania)

BBC

ADVERTISE HERE

More Stories

Manchester United yaendeleza mwenendo mbaya baada ya kichapo kutoka Chelsea
Manchester United yaendeleza mwenendo mbaya baada ya kichapo kutoka Chelsea
47m ago
READ MORE β†’
Gamondi aita kikosi cha kuikabili Nigeria kufuzu Afcon 2027
Gamondi aita kikosi cha kuikabili Nigeria kufuzu Afcon 2027
3h ago
READ MORE β†’
Ligi kuu bara kuendelea leo, Mkwakwani na Isamuhyo kuwaka moto
Ligi kuu bara kuendelea leo, Mkwakwani na Isamuhyo kuwaka moto
5h ago
READ MORE β†’
Dladla awataka mashabiki wa Yanga kujitokeza kwa wingi kuiunga mkono timu yao
Dladla awataka mashabiki wa Yanga kujitokeza kwa wingi kuiunga mkono timu yao
6h ago
READ MORE β†’
Tunatarajia mchezo mgumu, lakini lengo letu ni ubingwa: Dladla kocha yanga
Tunatarajia mchezo mgumu, lakini lengo letu ni ubingwa: Dladla kocha yanga
6h ago
READ MORE β†’
Wikiendi ya moto: Mechi kubwa sita kutawala viwanja vya soka
Wikiendi ya moto: Mechi kubwa sita kutawala viwanja vya soka
8h ago
READ MORE β†’
Jeraha la Kariakoo derby lamuondoa Duke Abuya Harambee stars
Jeraha la Kariakoo derby lamuondoa Duke Abuya Harambee stars
9h ago
READ MORE β†’
CAF yamchagua Arajiga miongoni mwa waamuzi 35 kupata mafunzo maalum Cairo
CAF yamchagua Arajiga miongoni mwa waamuzi 35 kupata mafunzo maalum Cairo
9h ago
READ MORE β†’
Hoja tano zinazoweza kuboresha tuzo ya Ballon d’Or
Hoja tano zinazoweza kuboresha tuzo ya Ballon d’Or
21h ago
READ MORE β†’
Samatta katika mtihani mzito: Le Havre ikiikaribisha PSG leo
Samatta katika mtihani mzito: Le Havre ikiikaribisha PSG leo
1d ago
READ MORE β†’