Tetesi za soka Ulaya, Jumatatu April 22 2024

Joel JJ By Joel JJ
β€’
22 Apr 2024
Tetesi za soka Ulaya, Jumatatu April 22 2024

Barcelona wana nia ya kumsajili mshambuliaji wa Liverpool mwenye umri wa miaka 27 raia wa Colombia Luis Diaz msimu huu wa joto. (Sport - kwa Kihispania)

Wolves inawazingatia kipa wa Arsenal Muingereza Aaron Ramsdale, 25, mlinda lango wa Liverpool na Jamhuri ya Ireland, Caoimhin Kelleher, 23, na kipa wa Sunderland Anthony Patterson kamawanaoweza kuziba nafasi ya kipa wa Ureno Jose Sa, 31, anayeondoka kutoka klabu hiyo msimu huu wa joto. (Sun)

Manchester City wako tayari kusikiliza ofa kwa kiungo wa kati wa Uingereza Jack Grealish mwenye umri wa miaka 28 msimu huu wa joto. (Football Insider)

Barcelona itasikiliza ofa kwa mlinzi wa Uruguay Ronald Araujo, 25, msimu huu, huku Manchester United ikionyesha nia. (Sport - kwa Kihispania, kupitia Goal)

Crystal Palace wanaweza kujiunga na harakati za kumsaka kiungo wa kati wa Club Bruges wa Nigeria Raphael Onyedika, 23. (Sun)

Arsenal, Liverpool na Manchester United ni miongoni mwa vilabu vinavyotaka kumsajili beki wa Real Madrid na Ufaransa Ferland Mendy, 28. (L'Equipe - kwa Kifaransa)

Borussia Dortmund italazimika kulipakiasi cha kuvunja rekodi ya klabu cha £35m iwapo wanataka kubadilisha mkopo wao kwa mlinzi wa Chelsea Mholanzi Ian Maatsen, 22, kuwa mkataba wa kudumu. (Mirror)

Manchester City wanakabiliwa na ushindani kutoka kwa Arsenal na Liverpool kumsajili beki wa kushoto wa Wolves wa Algeria Rayan Ait-Nouri. (Mirror)

Vilabu vingi vya Premier League vinafikiria kumnunua mshambuliaji wa Atletico Madrid Mhispania Samu Omorodion, 19, ambaye yuko kwa mkopo Alaves. (AS - kwa Kihispania)

Arsenal italazimika kulipa euro 60m (£51m) ikiwa wanataka kumsajili mshambuliaji wa Serbia Dusan Vlahovic mwenye umri wa miaka 24 kutoka Juventus msimu huu wa joto. (Tuttosport - kwa Kiitaliano)

Newcastle wanapanga kumnunua mlinzi wa Juventus mwenye umri wa miaka 19 wa Juventus Dean Huijsen ambaye kwa sasa yuko kwa mkopo Roma kwa pauni milioni 25. (Mirror)

Manchester United na Newcastle huenda zikamnunua kiungo wa kati wa Ufaransa Adrien Rabiot, 29, ikiwa hatasaini mkataba mpya na Juventus msimu huu wa joto. (Calciomercato - kwa Kiitaliano)

Leeds huenda ikakubali ofa ya karibu pauni milioni 30 kwa winga wa Italia Wilfried Gnonto, 20, ambaye anavutia vilabu kadha vya Premier League. (Football Insider)

BBC

ADVERTISE HERE

More Stories

Gamondi aita kikosi cha kuikabili Nigeria kufuzu Afcon 2027
Gamondi aita kikosi cha kuikabili Nigeria kufuzu Afcon 2027
51m ago
READ MORE β†’
Ligi kuu bara kuendelea leo, Mkwakwani na Isamuhyo kuwaka moto
Ligi kuu bara kuendelea leo, Mkwakwani na Isamuhyo kuwaka moto
2h ago
READ MORE β†’
Dladla awataka mashabiki wa Yanga kujitokeza kwa wingi kuiunga mkono timu yao
Dladla awataka mashabiki wa Yanga kujitokeza kwa wingi kuiunga mkono timu yao
3h ago
READ MORE β†’
Tunatarajia mchezo mgumu, lakini lengo letu ni ubingwa: Dladla kocha yanga
Tunatarajia mchezo mgumu, lakini lengo letu ni ubingwa: Dladla kocha yanga
4h ago
READ MORE β†’
Wikiendi ya moto: Mechi kubwa sita kutawala viwanja vya soka
Wikiendi ya moto: Mechi kubwa sita kutawala viwanja vya soka
5h ago
READ MORE β†’
Jeraha la Kariakoo derby lamuondoa Duke Abuya Harambee stars
Jeraha la Kariakoo derby lamuondoa Duke Abuya Harambee stars
6h ago
READ MORE β†’
CAF yamchagua Arajiga miongoni mwa waamuzi 35 kupata mafunzo maalum Cairo
CAF yamchagua Arajiga miongoni mwa waamuzi 35 kupata mafunzo maalum Cairo
6h ago
READ MORE β†’
Hoja tano zinazoweza kuboresha tuzo ya Ballon d’Or
Hoja tano zinazoweza kuboresha tuzo ya Ballon d’Or
19h ago
READ MORE β†’
Samatta katika mtihani mzito: Le Havre ikiikaribisha PSG leo
Samatta katika mtihani mzito: Le Havre ikiikaribisha PSG leo
1d ago
READ MORE β†’
Chelsea na Manchester united katika vita ya alama tatu kesho Stamford Bridge
Chelsea na Manchester united katika vita ya alama tatu kesho Stamford Bridge
1d ago
READ MORE β†’