Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya NBC Yanga leo wako Ruangwa mkoani Lindi kumenyana na Namungo Fc katika mwendelezo wa mikiki mikiki ya Ligi
Tangu ujio wa kocha Mwinyi Zahera, Namungo Fc imaimarika zaidi ikipoteza mchezo mmoja tu katika mechi tano zilizopita
Leo wanakutana na Yanga ambao alama tatu zitawahakikishia kurudi kileleni mwa msimamo wa ligi
Yanga ilitua Ruangwa jana kwa usafiri wa ndege ya kukodi wakipitia Nachingwea
Yanga leo inatarajiwa kuwakosa baadhi ya nyota wao muhimu akiwemo mlinda lango Djigui Diarra, viungo Khalid Aucho na Pacome Zouzoua pamoja na mlinzi wa kushoto Joyce Lomalisa
Wachezaji hao sio miongoni mwa waliosafiri na Yanga kutokana na changamoto za majeruhi na matatizo ya kifamilia
Mchezo utapigwa saa 12 jioni
ADVERTISE HERE