Simba yaomba kuhamia Zanzibar

Joel JJ By Joel JJ
β€’
30 Jan 2024
Simba yaomba kuhamia Zanzibar

Shirikisho la Soka Visiwani Zanzibar ZFF limekiri kupokea barua ya maombi kutoka kwa Klabu ya Simba ya kuomba kutumia uwanja wa New Aman sports Comlpex katika michezo ya nyumbani ya Ligi kuu, kombe la shirikisho la Azam (ASFA) na michezo iliyosalia ya hatua ya makundu klabu bingwa barani Afrika (CAF)

Akizungumza na CLOUDS MEDIA Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Visiwani Zanzibar Hussein Ahmada Vuai amesema kuwa leo Januari 29 mwaka 2024 wamepokea barua rasmi kutoka klabu ya Simba ya kuomba kutumia uwanja wa Amani katika michezo yake ya nyumbani kwa mashindano mbalimbali

"Nikiri kwamba leo ofisi yangu ya katibu Mkuu ZFF nimepokea barua rasmi kutoka kwa Klabu ya Simba ya Dar es Salam kuomba kutumia Uwanja wa New Aman Sports Comlpex katika michezo yake ya nyumbani baada ya Kiwanja cha Mkapa na Uhuru kufungiwa kupisha ukarabati"

"Sisi ZFF kwa upande wetu tumepokea barua hiyo kwa heshima kubwa kwa ndugu zetu Timu ya Simba na kwetu sisi tunaona ni jambo linaloweza kuleta faraja kwa mpira wa Zanzibar endapo litakwenda kufanikiwa kwa asilimia 100 na kufungua fursa kwa Wazanzibar na Watanzania wanaoishi visiwani humu kuiona Ligi kuu ya NBC na mashindano mengine kuchezwa "Zanzibar,” alisema Vuai

Msimamo wa Shirikisho la Soka Zanzibar kutoa ushirikiano kwa klabu ya Simba ili kufanikisha matakwa yao. Aidha amefafanua kuwa baada ya kupokea barua amechukua jitihada za kuzungumza na Meneja wa Uwanja, Bodi ya Ligi, Kamshna wa Idara ya Michezo na Wizara yenye dhamana na michezo Visiwani Zanzibar

"Baada ya kupokea barua sisi kama ZFF Jukumu letu ni kuweza kupeleka taarifa hizi katika vyombo ambavyo tunafanya navyo kazi kwa karibu kwa ajili ya kuweza kufanikisha hili"

ADVERTISE HERE

More Stories

Manchester United yaendeleza mwenendo mbaya baada ya kichapo kutoka Chelsea
Manchester United yaendeleza mwenendo mbaya baada ya kichapo kutoka Chelsea
47m ago
READ MORE β†’
Gamondi aita kikosi cha kuikabili Nigeria kufuzu Afcon 2027
Gamondi aita kikosi cha kuikabili Nigeria kufuzu Afcon 2027
3h ago
READ MORE β†’
Ligi kuu bara kuendelea leo, Mkwakwani na Isamuhyo kuwaka moto
Ligi kuu bara kuendelea leo, Mkwakwani na Isamuhyo kuwaka moto
5h ago
READ MORE β†’
Dladla awataka mashabiki wa Yanga kujitokeza kwa wingi kuiunga mkono timu yao
Dladla awataka mashabiki wa Yanga kujitokeza kwa wingi kuiunga mkono timu yao
6h ago
READ MORE β†’
Tunatarajia mchezo mgumu, lakini lengo letu ni ubingwa: Dladla kocha yanga
Tunatarajia mchezo mgumu, lakini lengo letu ni ubingwa: Dladla kocha yanga
6h ago
READ MORE β†’
Wikiendi ya moto: Mechi kubwa sita kutawala viwanja vya soka
Wikiendi ya moto: Mechi kubwa sita kutawala viwanja vya soka
8h ago
READ MORE β†’
Jeraha la Kariakoo derby lamuondoa Duke Abuya Harambee stars
Jeraha la Kariakoo derby lamuondoa Duke Abuya Harambee stars
9h ago
READ MORE β†’
CAF yamchagua Arajiga miongoni mwa waamuzi 35 kupata mafunzo maalum Cairo
CAF yamchagua Arajiga miongoni mwa waamuzi 35 kupata mafunzo maalum Cairo
9h ago
READ MORE β†’
Hoja tano zinazoweza kuboresha tuzo ya Ballon d’Or
Hoja tano zinazoweza kuboresha tuzo ya Ballon d’Or
21h ago
READ MORE β†’
Samatta katika mtihani mzito: Le Havre ikiikaribisha PSG leo
Samatta katika mtihani mzito: Le Havre ikiikaribisha PSG leo
1d ago
READ MORE β†’