Jana Mlandege Fc walitinga fainali ya Kombe la Mapinduzi kwa mwaka wa pili mfululizo baada ya kuitoa APR kwa mikwaju ya penalti 4-2
Dakika 90 za mchezo zilimalizika kwa suluhu, ingawa dakika 3 kabla kutimia dakika 90, Masoud Rashid Juma wa Mlandege FC na Clément Niyigena wa APR walioneshwa kadi nyekundu kwa mchezo usio wa kiungwana
Macho na masikio yametega kutaka kungámua, nani kucheza fainali na Mabingwa watetezi wa Mapinduzi? Je, watafanikiwa kutetea taji? Dakika 90’za mchezo wa leo majira ya saa 2:15 usiku zitaamua, ima Singida Fountain Gate au Simba SC kumenyana na watetea ubingwa
Simba na Singida wamepenya kutoka kundi moja. Mchezo wao wa siku 6 nyuma, Singida walikubali kichapo cha 0-2 dhidi ya mnyama
Historia itajirudia? Fainali ya msimu wa 17 wa Kombe la Mapinduzi, Singida walitinga hatua ya fainali na kukubali kipigo cha 1-2 kutoka kwa mabingwa watetezi, Mlandege FC mnamo Januari 13, 2023.